UTARATIBU WA KUPATA LESENI ZA BIASHARA
Leseni zote za Biashara hutolewa chini ya Sheria ya Biashara Na. 25 ya mwaka 1972 na marekebisho yake yaliyofanyika mwaka 1980. Mwombaji wa leseni ya biashara anapaswa ajaze fomu ya maombi ya leseni TFN 211 (Business license application form).
Leseni za Biashara zimegawanyika katika makundi mawili:
KUNDI A: Leseni hizi hutolewa na Wizara ya viwanda na Biashara ambazo ni;
•Uagizaji wa bidhaa toka nje (Import license)
•Kusafirisha bidhaa nje (Export license)
•Wakala wa mali (Estate Agent)
•Hotel za Kitalii (Tourist Hotel & Lodging)
•Wakala wa kupokea na usafirishaji mizigo (Clearing & Forwarding & Freight forwarders) nk.
KUNDI B: Hizi hutolewa na Halmashauri ya Jiji husika mfano:
•Wakala wa Bima (Insurance Agent) •Vipuri (Spare parts, Machine Tools) •Maduka ya dawa za binadamu/ Mifugo •Viwanda vidogo (Small scale manufacture and selling) •Uuzaji wa bidhaa Jumla na rejareja (Wholesale & Retail trade) n.k
MASHARTI YA KUOMBA NA KUPEWA LESENI ZA BIASHARA
i.Mfanyabiashara anapaswa awe na hati ya usajili iwapo anatumia jina la biashara (Certificate of Registration or Incorporation)
ii.Kama ni Kampuni mwombaji awe na “Memorandum of Article of Association” ambazo zinaonyesha kuwa kampuni imeruhusiwa kufanya biashara anayoiomba.
iii.Awe na mahali/ Eneo linalokubalika kwa aina ya biashara anayoiomba naisiwe vibanda vilivyopo kando kando ya barabara.
iv.Mfanyabishara aje na kivuli cha Cheti cha namba ya mlipa kodi (TIN) pamoja na kivuli cha cheti kinachoonyesha kuwa umelipa mapato kwa mujibu wa Sheria (Tax Clearance) ambavyo vyote vinatolewa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).
v.Masharti mengine ya kupata Leseni hutegemea aina ya biashara mtu anayetaka kuanzisha eg. Mgahawa inadidi afuate taratibu zote za afya na kupima wafanyakazi wake.
vi.Hati ya Utaalamu (Professional Certifucates) kwa biashara zote za kitaalam.
MALIPO
Serikali ilirudisha rasmi utoaji wa ada za leseni za biashara kupitia Sheria ya Fedha na 5 ya mwaka 2011. Kutokana na marekebisho hayo, Utaratibu wa kutoa leseni za biashara bila malipo uliondolewa na kurudishwa ada ya Leseni kuanzia tarehe 30 Juni, 2013.
Kiwango cha ada ya leseni kinatofautina kulingana na aina ya biashara husika na eneo ilipo biashara hiyo. Mfano: Kiwango cha ada za Lesseni kwa Halamshauri ya Jiji na Manispaa ni tofauti na za Halamshauri ya Wilaya na maeneo ya vijijini.
Baada ya ulipaji wa ada hiyo mfanyabiashara atapatiwa stakabadhi kwa malipo halali ya Fedha yake
Adhabu
Mnyabiashara atakayekutwa anafanya biashara bila kuwa na Leseni atatozwa faini ya kuanzia Shs 50,000/= - hadi 300,000/= au apelekwe mahakamani hii imeainishwa kutoka kifungu Na. 10 (1) (b).
WAJIBU WA MFANYABIASHARA
•Kulipia kila mwaka Lesseni ya Biashara yako kwa mujibu wa makadirio
•Ni jukumu la kila mfanyabishara kumiliki lesseni katika eneo lake la biashara na kuiweka mahala pa wazi ili kuonekana kwa urahisi.
AINA ZA LESENI
i.Leseni za vileo
Biashara ya vileo inatekelezwa kwa kufuata Sheria ya mwaka 1968, Kifungu 28 (Liquor License Act No. 28 of 1968) na marekebisho ya sheria hiyo yaliyofanywa mwaka 2004.
UTARATIBU WA UPATIKANAJI WA LESENI
Maombi yote mapya ya Leeseni za vileo ni lazima yapitishwe na wataalam ambao wameainishwa kwenye Fomu ya maombi (Afisa Biashara, Ardhi, Afisa Biashara, Polisi na Mwenyekiti wa Kamati ya maendeleo ya Kata husika.
Maombi yote yanayorudiwa (Renewal) yawasilishwe moja kwa moja kwa Afisa biashara anayeshughulikia leseni za vileo kwa utekelezaji.
Leseni za vileo hutolewa kwa vipindi viwili (2) ambapo kipindi cha kwanza huanzia tarehe 1/04 hadi 30/09 na kipindi cha pili huanzia tarehe 1/10 hadi 31/03 mwaka unaofuata.
ADA:
Maombi mapya na yanayorudiwa hulipiwa ada ya Jumla ya Tsh. 40,000 – kwa wale wanaouza pombe katika maeneo yao ya biashara (Retailers On) na ada ya fomu Tsh 2,000/= na kwa wale wanaouza Pombe za Kienyeji hulipia ada ya Tsh. 12,000/=
Aidha wanaoendesha biashara ya vileo bila kufuat taratibu zilizotajwa hapo juu huchukuliwa hatua za kisheria ikiwa ni pamoja na kupelekwa Mahakamani kulipishwa faini pamoja na penalty au kufungiwa biashara zao.
ii.Leseni za biashara mbalimbali
Lesseni hii inatolewa chini ya sheria namba 25 ya mwaka 1972 na marekebisho yake ya mwaka 1980.
FAIDA ZA MFANYA BIASHARA KUWA NA LESENI NI PAMOJA NA:
•Kutambulika kama mfanya bihashara halali
•Husaidia kupata mikopo mbalimbali
•Husaidia kupata fursa mbalimbali za kibiashara
•Kuchangia katika uchumi wa Taifa (Ada)
•Kuepuka usumbufu wa kufungiwa Biashara kwa kutokuwa na leseni halali.
Buchosa District Council
Anuani: 44 Buchosa - SENGEREMA
Simu: 0759941297
Simu ya kiganjani: 0765029662
Barua pepe: ded@buchosadc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Hamlashauri ya Wilaya ya Buchosa. Haki zote zimehifadhiwa