Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Buchosa afanya kikao na watumishi wa Halmashauri makao makuu awataka ushirikiano katika ukusanyaji wa mapato.
Mkurugenzi wa Halmashauri Wilaya ya Buchosa Bw.Benson Mihayo amefanya kikao leo tarehe 27,Machi,2025, katika ukumbi wa mikutano wa halmashauri na Watumishi wa Makao makuu ikiwa ni utaratibu wake wa kawaida aliojiwekea wa kuongea na watumishi kila robo ya mwaka ambapo amesikiliza kero na changamoto mbalimbali zinazowakabili watumishi ikiwa ni pamoja na uhaba wa vitendea kazi, pamoja na madeni ya watumishi.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri amewataka watumishi wa makao makuu kushirikiana kwa pamoja katika juhudi za ukusanyaji wa mapato ambapo ameeleza kuwa mpaka sasa hali ya ukusanyaji wa mapato katika Halmashauri ya Buchosa unaenda vizuri.
Aidha Bw. Mihayo ameeleza na kufafanua kwamba atahakikisha kila mtumishi anapata stahiki zake za msingi ikiwa pamoja na kulipa fedha za madeni ya uhamisho,likizo kulingana na bajeti ya halmashauri itakavyokuwa inaimarika.
Kwa upande wake Kaimu Afisa Utumishi Bi.Jackline George amewataka watumishi kuendelea kufaya kazi kwa juhudi na kwenye mfumo wa PEPMIS ili kuendana na kasi iliyopo na kila mtu atimize majukumu kwa nafasi yake ambapo amesisitiza kwamba wafanyakazi Hodari watapatikana kwa kufanya kazi kwenye mfumo wa PEPMIS na kila mtumishi angalau awe amefikisha asilimia 75.
Kwa upande wao watumishi wamefurahishwa na kitendo cha Mkurugenzi Mtendaji cha kuwa na utaratibu wa kuongea na watumishi na kusilizwa kero na changamoto zao kutatuliwa.
Buchosa District Council
Anuani: 44 Buchosa - SENGEREMA
Simu: 0759941297
Simu ya kiganjani: 0765029662
Barua pepe: ded@buchosadc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Hamlashauri ya Wilaya ya Buchosa. Haki zote zimehifadhiwa