Halmashauri ya Buchosa imeadhimisha siku ya kuzaliwa ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kufanya zoezi la upandaji wa miti ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono juhudi za kitaifa za uhifadhi wa mazingira na mapambano dhidi ya mabadiliko ya tabianchi.
Mwenyeki wa Halmashauri ya Buchosa Mhe. Isaac Mashimba leo ameongoza zoezi la upandaji miti katika Shule ya Msingi Nyamadoke ilipo Kata ya Nyamadoke,ikiwa ni sehemu ya kampeni ya kitaifa ambayo inalenga kulinda mazingira, na kuhimiza matumizi ya Nishati safi ya kupikia, ushirikiano kati ya Serikali na Wananchi katika kuhakikisha mipango hiyo inatekelezwa kwa ufanisi.
Aidha jumla ya miti 3,100 imepandwa maeneo mbalimbali ikiwa ni pamoja na Shule ya Msingi Nyamadoke,Shule ya Msingi Kasisa,Shule ya Msingi Misungwi,Shule ya Msingi Nyehunge,Shule ya Sekondari Kalebezo,Nyanango Sekondari ikiwa ni sehemu ya kuungana na Mhe. Rais Dkt Samia Suluhu Hassan katika kusheherekea siku yake ya kuzaliwa kwa kutunza mazingira.
Hata hivyo upandaji Miti umefanyika kwa kushirikisha Viongozi mbalimbali wakiwemo Wataalamu wa Misitu,Viongozi,Wakuu wa Idara na Vitengo,Walimu na Wanafunzi pamoja na Wananchi.
Buchosa District Council
Anuani: 44 Buchosa - SENGEREMA
Simu: 0759941297
Simu ya kiganjani: 0765029662
Barua pepe: ded@buchosadc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Hamlashauri ya Wilaya ya Buchosa. Haki zote zimehifadhiwa