Baraza la Madiwani Halmashauri ya Wilaya ya Buchosa latoa mikakati ya kuwatumikia wananchi ikiwa kipaumbele ni kuhakikisha ukusanyaji wa mapato unaongezeka.
Katika mkutano wa kwanza wa baraza hilo, Waheshimiwa Madiwani wamefanya uchaguzi wa viongozi katika kamati mbalimbali ambapo Mhe. Isaac Mashimba, Diwani wa Kata ya Kalebezo amechaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Buchosa naye Mhe. Samike Hezron, Diwani wa Kata ya Luharanyonga, amechaguliwa kuwa Makamu Mwenyekiti.
Mhe.Mashimba amewashukuru waheshimiwa madiwani mara baada ya kuchaguliwa kwa kura zote za ndiyo kwa imani waliyoonyesha na kuahidi kuwa kiongozi atakayefika moja kwa moja kwa wananchi kusikiliza na kuwasilisha kero zao.Ameahidi Baraza hilo kwamba atahakikisha rasilimali zinasimamiwa vizuri na kwa usawa sambamba na hilo atahakikisha anasimamia maslahi ya wananchi na watumishi kwa ujumla.
Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Buchosa Mhe.Erick Shigongo amewashukuru Waheshimiwa Madiwani,Mkurugenzi Mtendaji na Watumishi kuwa wamoja kipindi cha uchaguzi hadi kufikia leo na kuahidi kutoa ushirikiano kwa maslahi ya wananchi na Taifa kwa ujumla.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Buchosa ameeleza na kufafanua kwamba atashirikiana na waheshimiwa Madiwani katika kuhakikisha kuwa uchumi imara na endelevu na jamii iliyoelimika yenye maisha bora na inayowajibika katika maendeleo.
“Sisi ni wanabuchosa tutaijenga wenyewe,nimekuja Buchosa kutoa huduma na si kutawala”Amesisitiza Bw.Mihayo.
Mkutano wa kwanza wa baraza la Madiwani umehudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo Katibu Tawala Wilaya ya Sengerema Bw.Cuthbert Midala, viongozi wa vyama vya siasa, wakuu wa idara na Vitengo na wadau kama NMB na CRDB pamoja na wananchi.




Buchosa District Council
Anuani: 44 Buchosa - SENGEREMA
Simu: 0759941297
Simu ya kiganjani: 0765029662
Barua pepe: ded@buchosadc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Hamlashauri ya Wilaya ya Buchosa. Haki zote zimehifadhiwa