Menejimenti ya Halmashauri ya imefanya kikao kazi cha kupitia Mpango Mkakati wa Miaka Mitano (2021/2022–2025/2026) unaoishia Juni 2026 na kuanza maandalizi ya Mpango Mkakati Mpya wa Miaka Mitano (2026/2027–2030/2031).
Kikao kazi hicho, kinachohusisha Menejimenti ya Halmasahuri ya Buchosa kimeanza tarehe 13 hadi 15 Januari, 2026 katika Ukumbi mdogo wa mikutano wa Mkurugenzi kikiongozwa na Mwezeshaji ni ambaye ni Mhadhiri mwandamizi kutoka chuo cha serikali za mitaa Hombolo Dodoma Bw. Boaz Mbundu.
Akifungua mafunzo hayo Kaimu Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ambaye pia ni Mkuu wa Divisheni ya Mipango Ndg. Deogratius Lihengelimo, ameeleza na kufafanua kwamba kuandaa mipango mikakati thabiti itakaotengeneza Dira na maono ya halmashauri ili kufikia malengo ambayo yatakwenda kuibadilisha halmashauri katika nyanja zote za kiuchumi, miundombinu na kijamii kufikia Dira ya 2050.
Aidha lengo la kikao kazi hicho ni kutathmini mafanikio na changamoto za Mpango Mkakati unaoisha, pamoja na kuweka malengo na mikakati mipya itakayoongeza ufanisi na matokeo chanya kwa taasisi.
Hata hivyo Bw. Lihengelimo amesisitiza kuwa mpango huo ndio utafanya utekelezaji bora wa maandalizi ya bajeti mpya kwa mwaka 2026/2027.
Buchosa District Council
Anuani: 44 Buchosa - SENGEREMA
Simu: 0759941297
Simu ya kiganjani: 0765029662
Barua pepe: ded@buchosadc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Hamlashauri ya Wilaya ya Buchosa. Haki zote zimehifadhiwa