Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Buchosa afanya kikao na watumishi wa Halmashauri makao makuu, awataka kuendelea kuzingatia majukumu yao ya kazi pamoja na kudumisha amani na upendo.
Mkurugenzi wa Halmashauri Wilaya ya Buchosa Bw.Benson Mihayo amefanya kikao leo tarehe 28,Novemba,2025, katika ukumbi wa mikutano wa halmashauri cha watumishi wa makao makuu ambapo wamewataka watumishi kutimiza majukumu yao ya kazi kwa kushirikiana kwa pamoja ili kudumisha amani na upendo katika kazi.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ameeleza na kufafanua kwamba watumishi wanaodai stahizi zao mbalimbali kama madeni ya uhamisho Halmashauri imeshalipa watumishi wake kwa asilimia kubwa na kuahidi kuendelea kulipa madeni kwa watumishi ambao bado wanadai ili kuondoa changamoto hizo zinazowakabili watumishi.
Aidha Bw.Mihayo amewataka watumishi kuendelea kufaya kazi kwa juhudi na kwenye mfumo wa PEPMIS kuendana asilimia zinazohitajika pindi wanapotimiza majukumu yao kwenye mfumo.
Hata hivyo Mkurugenzi Mtendaji amewakumbusha watumishi kuendelea kutimiza majukumu yao kama kawaida na kutokujihusiha na makundi ambayo yanaweza kuchochea vurugu na kuchafua amani ya nchi yetu.


Buchosa District Council
Anuani: 44 Buchosa - SENGEREMA
Simu: 0759941297
Simu ya kiganjani: 0765029662
Barua pepe: ded@buchosadc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Hamlashauri ya Wilaya ya Buchosa. Haki zote zimehifadhiwa