Halmashauri ya Wilaya ya Buchosa yatoa mafunzo kwa watumishi wa ajira mpya ili kuwajengea uwezo na uelewa wa pamoja kuhusu masuala mabalimbali katika Utumishi wa umma.
Mafunzo hayo ya kuwajengea uwezo watumishi yametolewa leo tarehe 19, Novemba, 2025 katika ofisi za Halmashauri ambapo wameelekezwa kuzingatia maadili ya utumishi wa umma pamoja na sheria,kanuni na taratibu pindi wanapotimiza majukumu yao ya kazi.
Aidha mada zilizofundishwa ni pamoja Haki na wajibu wa wa mtumishi wa Umma, maadili na mwenendo kwa mtumishi, makosa ya kiutumishi na adhabu zake, na maadili katika utumishi wa umma.




Buchosa District Council
Anuani: 44 Buchosa - SENGEREMA
Simu: 0759941297
Simu ya kiganjani: 0765029662
Barua pepe: ded@buchosadc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Hamlashauri ya Wilaya ya Buchosa. Haki zote zimehifadhiwa