Watumishi pamoja na Wafanyabiashara wajitokeza kwa kufanya usafi katika soko la Nyehunge Halmashauri ya Wilaya ya Buchosa Mkoani Mwanza.
Zoezi hilo limefanyika leo mapema 28, Februari, 2025 katika Soko la Nyehunge ambapo watumishi wa kada mbalimbali wamehudhuria na kushiri kufanya usafi maeneo yote yanayo zunguka soko hilo ikiwa ni utaratibu wa kawaida wa kufanya usafi kila siku ya Ijumaa ya mwisho wa mwezi.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Buchosa ambaye pia ni Mganga Mkuu wa Wilaya Daktari David Mndeba ameeleza na kufafanua kwamba zoezi hilo la kufanya usafi lipaswa kufanyika kila siku katika maeneo yetu na maeneo mengine ya taasisi ili kuepukana magonjwa.
“Usafi huu utakuwa mwendelezo wa kila siku ya Ijumaa ya mwisho wa mwezi lakini usafi ni tabia ya mtu,papende pale unapofanyia kazi zako mazingira yawe safi”.
“watumishi tushiriki wote kwenye usafi ambalo ni agizo la Serikali”amesisitiza Mgaga Mkuu wa Wilaya.
Aidha Dkt Mndeba ametoa wito kwa watumishi kujitokeza kwa wingi katika matukio kama haya ili kuwa mfano wa kuigwa kwa wananchi sambasamba na kufanya usafi katika maeneo yao wanakoishi.
Buchosa District Council
Anuani: 44 Buchosa - SENGEREMA
Simu: 0759941297
Simu ya kiganjani: 0765029662
Barua pepe: ded@buchosadc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Hamlashauri ya Wilaya ya Buchosa. Haki zote zimehifadhiwa