Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) watakiwa kuongeza kasi kuboresha miundombinu ya Barabara katika Halmashauri ya Buchosa wilayani Sengerema Mkoani Mwanza.
Wito huo umetolewa tarehe 11, Febrary,2026 na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Buchosa Mhe.Isack Mashimba katika Baraza la Madiwani wakati wa kujadili na kupitisha mapendekezo ya Bajeti ya Mapato na Matumizi ya shilingi Bilioni 44.7 kwa mwaka wa fedha 2026/2027 katika Halmashauri Buchosa.
Mhe.Mashimba ameeleza kufafanua kwamba TARURA wanaojibu wa kuhakikisha wanaboresha miundombinu ya barabara za mitaa kwa wakati ili ziweze kupitika kwa urahisi na watumiaji wa barabara hizo ambapo zitachochea maendeleo ya kijamii na kiuchumi kwa wakazi wa buchosa.
Kwa upande wao Waheshimiwa Diwani wa Halmashauri ya Buchosa wameeleza na kusisitiza umuhimu wa kupewa kipaumbele katika bajeti ya TARURA ili kuboresha mtandao wa barabara katika Kata za Halmashauri ya Buchosa.
Hata hivyo, Meneja wa Wakala wa Barabara za mijiji na Vijiji (TARURA) Wilaya ya Sengerema, Bw.Prosper Francis amesema kwamba watahakikisha barabara za Halmashauri ya Buchosa zinaboresha kwa kiwango kinachokubalika.Sambamba na kuahidi kuendeleza ushirikiano na Halmashauri kwa kutatua changamoto zinazojitokeza.



Buchosa District Council
Anuani: 44 Buchosa - SENGEREMA
Simu: 0759941297
Simu ya kiganjani: 0765029662
Barua pepe: ded@buchosadc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Hamlashauri ya Wilaya ya Buchosa. Haki zote zimehifadhiwa