Baraza la Wafanyakazi la Halmashauri ya Wilaya ya Buchosa lajadili na kupitisha mapendekezo ya Bajeti ya Mapato na Matumizi ya shilingi Bilioni 44.7 kwa mwaka wa fedha 2026/2027 katika Halmashauri Buchosa Mkoani Mwanza.
Akiwasilisha rasimu hiyo ya Bajeti kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji Bw. Deogratius Lihengelimo ambaye ni Mkuu wa divisheni ya Mipango na uratibu ameeleza na kufafanua kwamba Halmashauri ya Buchosa kwa Mwaka wa fedha 2026/2027 inategemea kukusanya na kutumia jumla ya Shilingi 44,770,074,000.00 kutoka vyanzo mbalimbali vya halmashauri.
Katika fedha hizo shilingi 28,170,112,000.00 ni Ruzuku kutoka Serikali Kuu kwa ajili ya mishahara, Shilingi 1,853,182,000.00 ni Matumizi mengineyo, Shilingi 5,447,179,000.00 ni mapato ya ndani ya halmashauri na Shilingi 9,299,601,000.00 ni ruzuku ya Miradi ya Maendeleo.
Aidha kiasi cha makusanyo kimeongezeka kwa silimia 3.46 ukilinganisha na Mwaka wa fedha 2025/2026 ambapo makisio yalikuwa ni shilingi 5,264,979,000.00 hii imetokana na halmashauri kuweka mikakati madhubuti ya kukusanya mapato.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali za Mitaa TALGWU Bw. Mkama Sululu ameipongeza halmashauri kwa kuandaa rasimu ya bajeti nzuri ambayo imezingatia maslahi ya watumishi kwa kiasi kubwa ikiwemo kulipa madeni ya watumishi na uhamisho.
Naye Mwenyekiti wa chama cha Waalimu (CWT) Wilaya ya Sengerema Bw. Zacharia Mganda amempongeza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Buchosa Bw.Benson Peter Mihayo kwa kushirikiana na Timu Menejimenti ya halmashauri kwa kuandaa rasimu ya bajeti inayofaa kwa imezingatia maslahi ya watumishi wa umma.
Hata hivyo, kupitia kikao hicho cha Baraza la Wafanyakazi, wajumbe walipata wasaa wa kupitia na kujadili pamoja na kutoa maoni yao juu ya Bajeti hiyo na kupongeza namna ilivyoandaliwa kitaalamu.
Buchosa District Council
Anuani: 44 Buchosa - SENGEREMA
Simu: 0759941297
Simu ya kiganjani: 0765029662
Barua pepe: ded@buchosadc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Hamlashauri ya Wilaya ya Buchosa. Haki zote zimehifadhiwa