Mkuu wa Wilaya ya Sengerema Mhe.Senyi Ngaga awataka Wanawake kumuunga mkono Mhe.Rais Dkt Samia Suluhu Hassan katika miradi ya Maendeleo katika Halmashauri ya Buchosa.
Mheshimiwa Ngaga ameyabainisha hayo leo tarehe 7, Machi,2025 wakati wa Maadhimisho siku ya Wanawake duniani yaliyofanyika Kiwilaya Buchosa katika viwanja vya Nyehunge ambapo ametoa wito kwa wanawake wote kuendelea kujituma na kufanya kazi kwa bidii katika kutekeleza miradi mbali mbali ambayo inatekelezwa na Serikali ili kuleta tija na kuharakisha maendeleo kwa Wananchi.
Amesema Serikali imetoa fedha kiasi cha shilingi 485,000,000 kwa ajili ya mikopo ya asilimia 10 ya Wanawake,Vijana na watu wenye ulemavu ambapo ametoa rai kwa wanawake ambao watabahatika kupata mikopo hiyo waweze kurejesha kwa wakati ili na watu wengine waweze kukopa.
“Ni mikopo ambayo haina riba lakini siyo fedha ambazo zinatolewa bure, lazima turejeshe na tunavyorejesha tunafanya kapu letu la Buchosa linazidi kujaa”amesema Bi.Ngaga.
Ngaga amewataka wanawake kutumia vizuri mikopo wanayo kopeshwa na Serikali iwe yenye kuleta tija na kukuza kipato na kuongeza ajira kwa watu wengine na kabla kupatiwa fedha hizo wapewe elimu ya namna ya kutumia fedha hizo.
Aidha Mkuu wa Wilaya ametoa wito kwa wanawake kujiamini na kugombea nafasi mbalimbali za uongozi katika taifa hili kwani nafasi bado zipo wazi kwa ajili ya wanawake.
“Nategemea nikiwaona wanawake tukijitokeza katika vinyang’anyiro mbalimbali vya uongozi pale muda utakapofika,twendeni tukagombee”amesisitiza Mkuu wa Wilaya Mhe.Senyi Ngaga.
Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Buchosa Mhe.Erick Shigongo ameeleza na kufafanua kwamba Serikali ya awamu ya sita imeendelea kuthamini michango ya wanawake katika jamii na kuwataka Wanawake kuendelea kudai haki zao za msingi na kusisitiza kwamba wanawake wakiendelezwa jamii nzima imeendelezwa.
Hata hivo Shigongo ametoa zawadi kwa wanafunzi wenye mahitaji Maalumu katika Shule ya Msingi Nyehunge ambapo ametoa shuka100.
Katika hatua nyingine sherehe hizo za Wanawake ziliambatana na utoaji wa zawadi katika Shule ya Msingi Nyehunge ambapo pia waliweza kutoa zawadi kwa wanafunzi wenye mahitaji maalumu kama vile sukari.
Maadhimisho hayo yaliambatana na kaulimbiu inayosema “Wanawake na Wasichana 2025 Tuimarishe haki,Usawa na Uwezeshaji”.
Buchosa District Council
Anuani: 44 Buchosa - SENGEREMA
Simu: 0759941297
Simu ya kiganjani: 0765029662
Barua pepe: ded@buchosadc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Hamlashauri ya Wilaya ya Buchosa. Haki zote zimehifadhiwa