Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Buchosa Bw.Deogratius Lihengelimo amekabidhi fomu za Uteuzi wagombea wa nafasi ya Ubunge Jimbo la Buchosa kupitia Chama Makini na Chama cha Sauti ya Umma (SAU).
Aidha wagombea hao ni pamoja na Bi.Consolata C.Mtalyantula kupitia Chama cha Sauti ya Umma na Bi.Elizabeth D.Msallamo kuptia Chama Makini ambapo makabidhiano hayo yamefanyika katika Ofisi ya Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Buchosa iliyopo Ofisi za Halmashauri ya Wilaya ya Buchosa.
Zoezi la Utoaji wa fomu za Uteuzi kwa wagombea nafasi za Ubunge na Udiwani bado linaendelea.
Kaulimbiu: "Kura yako Haki yako Jitokeze Kupiga Kura"
Buchosa District Council
Anuani: 44 Buchosa - SENGEREMA
Simu: 0759941297
Simu ya kiganjani: 0765029662
Barua pepe: ded@buchosadc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Hamlashauri ya Wilaya ya Buchosa. Haki zote zimehifadhiwa