Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Buchosa amewataka Vikundi vya ujasiriamali ambavyo ni Wanawake,Vijana na Watu wenye ulemavu kuwa na nidhamu ya fedha wakati wanapokopeshwa fedha kwa ajili kufanya biashara ili kufikia malengo waliyojiwekea.
Wito huo ametolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Buchosa leo tarehe 28,Agosti,2024 katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri wakati wa kuhitimisha mafunzo ya Vikundi hivyo ambapo amewataka kuwa waminifu, sambamba na kufanya tathmini kwenye biashara zao na kuwa na maono ya mbali ya kibiarasha yenye kuleta tija ili kujikwamua kiuchumi.
Aidha amesisitiza kwamba vikundi vinatakiwa kurejesha fedha walizokopeshwa bila riba kwa wakati ili na vikundi vingine vyenye sifa viweze kukopa.
Jumla ya vikundi 40 wemepatiwa mkopo wa asilimia 10 fedha kutoka mapato ya ndani ya Halmashauri ambapo vikundi (23) vya wanawake wamekopesha kiasi cha shilingi Milioni 106, Vijana vikundi (16) wamekopeshwa shilingi Milioni 241.5 na Watu wenye ulemavu ni kikundi kimoja kimekopesha shilingi Milioni (3) tatu na kufanya jumla ya shilingi 350,517,000/= ambazo zimekopeshwa kwa robo ya tatu mwaka wa fedha 2024/2025.
Buchosa District Council
Anuani: 44 Buchosa - SENGEREMA
Simu: 0759941297
Simu ya kiganjani: 0765029662
Barua pepe: ded@buchosadc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Hamlashauri ya Wilaya ya Buchosa. Haki zote zimehifadhiwa