Watumishi wa kada mbalimbali pamoja na Wananchi wajitokeza kwa wingi kufanya usafi katika Kituo cha Afya Nyuhunge ikiwa ni kuadhimisha siku ya Mashujaa Wilayani Buchosa mkoani Mwanza.
Zoezi hilo limefanyika leo mapema 25, Julai, 2024 katika Kituo cha Afya Nyehunge Kata ya Nyehunge ambapo watumishi wa kada mbalimbali wamehudhuria na kushiri kufanya usafi maeneo yote yanayo zunguka kituo hicho ikiwa ni kuadhimisha siku ya Mashujaa ambayo hufanyika tarehe 25, Julai kila mwaka.
Afisa Utumishi Mkuu wa Halmashauri ya Wilaya ya Buchosa Bw.Ritte Adolph ameeleza na kufafanua kwamba zoezi hilo la kufanya usafi linaenda sambamba na kuwambuka mashujaa wetu na kukumbushana sisi kuwa wazalendo kwa kuipenda nchi yetu kujituma kwa bidii katika kufanya kazi.
Aidha Bw.Adolph ametoa wito kwa watumishi kujitokeza kwa wingi katika matukio kama haya ili kuwa mfano wa kuigwa kwa wananchi sambasamba na kufanya usafi katika maeneo yao wanakoishi.
Tanzania huadhimisha siku ya kuwakumbuka Mashujaa waliopoteza maisha yao wakiutetea,kuupigania na kuulinda uhuru wa Tanzania kila ifikapo Julai,25 ya kila mwaka.
Watumishi kutoka Kada mbalimbali wa Halmashauri ya Wilaya ya Buchosa wajitokeza na kushiriki kufanya usafi leo mapema katika Kituo cha Afya Nyehunge ikiwa ni kuadhimisha siku ya Mashujaa ambayo hufanyika kila tarehe 25,Julai kila mwaka.
Buchosa District Council
Anuani: 44 Buchosa - SENGEREMA
Simu: 0759941297
Simu ya kiganjani: 0765029662
Barua pepe: ded@buchosadc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Hamlashauri ya Wilaya ya Buchosa. Haki zote zimehifadhiwa