Wathibiti Ubora ngazi ya Halmashauri wametakiwa kuweka malengo thabiti katika ufundishaji na ujifunzaji ili kuongeza ufanisi wa kazi za timu za ndani za uthibiti ubora wa shule katika kupanga na kuboresha mikakati katika elimu.
Akizungumza katika ufunguzi wa mafunzo ya Wathibiti Ubora wa Shule leo tarehe 30, Septemba,2025 katika ukumbi wa shule ya Sekondari Nyehunge Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Buchosa Bw.Benson Peter Mihayo,amewataka Wathibiti Ubora wa Shule kujijengea utamaduni wa kufundisha kwa bidii kukuza uwajibikaji ,uwazi kwa kushirikiana kwa pamoja ili kuongeza ufaulu katika sekta ya elimu.
“Tengenezeni utamaduni wa kufundisha kwa bidii ili kufikia malengo ya ufaulu ambayo mmejiwekea katika Shule zenu” amesema Mkurugenzi Mtendaji Bw.Benson Mihayo.
Kwa upande wake Uthibiti Ubora wa Shule Halmashauri ya Wilaya ya Buchosa Bi.Tunu M.Sarungi ameeleza na kufafanua kwamba mafunzo hayo ambayo yameandaliwa kwa lengo la kuwajengea uwezo Maafisa elimu kata, Wakuu wa shule,Wataalumu wakuu,pamoja na wenyeviti wa timu za uthibiti ubora wa shule za ndani ambapo wataweza kusimamia na kufuatilia viwango vya ubora wa elimu katika maeneo yao ya kazi.
Naye Afisa Elimu Sekondari Halmashauri ya Wilaya ya Buchosa Bw.Simbanilo Changiki amesema kuwa Mafuzo ya Wathibiti Ubora wa Shule yatasaidia timu hizo kuongeza ufanisi wa kuinua taaluma na maendeleo katika Sekta ya Elimu sambamba na kuongeza ubora wa ufundishaji na ujifunzaji shuleni.
Aidha mafunzo hayo yamewajengea uwezo Maafisa elimu kata, Wakuu wa Shule,Wataaluma wakuu na wenyeviti watimu za ndani katika kuhakikisha wanatambua majukumu yao na kusimamia ufaulu wa wanafunzi katika Halmashauri ya Wilaya ya Buchosa.
Buchosa District Council
Anuani: 44 Buchosa - SENGEREMA
Simu: 0759941297
Simu ya kiganjani: 0765029662
Barua pepe: ded@buchosadc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Hamlashauri ya Wilaya ya Buchosa. Haki zote zimehifadhiwa