Watendaji wa Kata na Vijiji wa wapigwa msasa namna bora ya usimamizi wa Mapato ili kuongeza tija na kasi katika ukusanyaji mapato katika Halmashauri ya Wilaya ya Buchosa Mkoani Mwanza.
Hayo yamefanyika leo 15, Julai, 2024 katika kikao kazi cha Watendaji wa Kata na Vijiji katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ambapo watendaji wametakiwa kusimamia sheria na kanuni na taratibu za usimamizi na ukusanyaji wa mapato kupitia Biashara,Viwanda,Masoko na Uwekezaji pamoja na Usafi ili kuondoa migogoro baina ya wafanya biashara na wakusanyaji wa mapato pindi wanapotimiza majukumu yao.
Akiongea katika kikao hicho Kaimu Mkurugenzi mtendaji wa Halmasahuri ya Wilaya ya Buchosa Bw.Ritte Adolph ambaye pia ni Afisa Utumishi amewataka Watendaji wa Kata na Vijiji kuendelea kufanya kazi kwa kushirikiana kwa pamoja pindi wapotimiza majukumu yao ya kila siku na kufuata taratibu sheria na kanuni za kazi ikiwa pamoja na usimamizi wa ukusanyaji wa mapato.
Aidha Bw.Adolph amekea baadhi ya tabia za watendaji wa Kata na Vijiji ambao wanakiuka sheria kanunni taratibu za kazi ikiwa pamoja na kutokukaa kwenye vituo vya kazi na kuwataka kuacha tabia hiyo na badala yake wawe na mawasiliano madhubuti ya wao kwa wao ili kurahisisha utendaji wa kazi katika vituo vyao.
Kwa upande wake Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Biashara Viwanda na Uwekezaji ametoa elimu kwa watendaji hao na kuwataka kwenda kusimamia vyema Sheria hiyo ya biashara pindi wanaposimamia utekelezaji wa ukusanyaji wa mapato katika kukagua leseni,kuwatambua na kuwasajili wafanyabiashara kwenye kanzi data ya Halmashauri katika maeneo wanakoishi.
Bw.Mkoba amesema wafanyabiashara wanatakiwa kuwa wazalendo kwa kulipa kodi,ada ya leseni ya biashara na ushuru kwa mujibu wa sheria kwa kufanya hivyo watachangia kuleta maendeleo katika jamii na Taifa kwa ujumla.
Naye Kaimu Afisa Maendeleo ya Jamii wa Halmashauri ya Wilaya ya Buchosa Bi.Grace Machunda amesema kwamba Serikali imedhamiria kuwainua wafanyabiashara wadogo wenye mapato chini ya milioni nne kwa mwaka kwa kuwapatia vitambulisho ambavyo vitakuwa vina vielelezo vyote muhimu vya Mjasiriamali mdogo ambavyo vitawaezesha kukopesheka katika taasisi za Benki,na kitambulisho hicho kitalipiwa shilingi elfu ishirini kwa muda kwa miaka mitatu na baada ya miaka mitatu atalipa 5000 kwa kuhuisha na kutumika miaka mitatu tena.
Kwa upande mwingine Afisa Afya Mazingira wa Halmashauri ya Wilaya ya Buchosa Bw. Norbert Aloyce Amworo ameeleza na kufafanua kuwa Watendaji wanaowajibu wa kusimamia na kuvilinda vyanzo vya maji,mialo,uoto wa asili pamoja na kusimamia usafi wa mazingira katika mazingira wanakoishi ili kuepusha magonjwa mbalimbali ambayo yanaweza kuzuilika.
Mtendaji wa Kata ya Maisome Bw.Albert Njigile Tumbo akiongea kwa niaba ya watendaji wote wa Halmashauri ya Wilaya Buchosa amesema wako tayari kutoa ushirikiano kwa timu ya ukusanyaji wa mapato kutoka makao makuu kutoka Halmashauri pindi wanapohitajika katika vituo vyao vya kazi.
Watendaji wa Kata na Vijiji wakisikiliza na kupokea maelekezo kutoka kwa Mkurugenzi Mtentandaji wakati wa kikao kazi katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri leo 15,Julai,2024.
Buchosa District Council
Anuani: 44 Buchosa - SENGEREMA
Simu: 0759941297
Simu ya kiganjani: 0765029662
Barua pepe: ded@buchosadc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Hamlashauri ya Wilaya ya Buchosa. Haki zote zimehifadhiwa