Waatalamu wa Sekta ya Elimu ngazi ya Halmashauri wametakiwa kuendena na mfumo wa kidijiti ili kuongeza ufanisi wa kazi za timu za ndani za uthibiti ubora wa shule katika kupanga na kuboresha mikakati katika elimu.
Akizungumza katika mafunzo hayo ya mfumo wa Kidijiti leo tarehe 11, Julai,2025 katika ukumbi wa shule ya Sekondari Nyehunge Bw.Simbanilo Changiki Afisa Elimu Sekondari Halmashauri ya Wilaya ya Buchosa ambaye amemwakilisha Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Buchosa Bw.Benson Peter Mihayo,amewataka Waatalamu wa sekta ya Elimu kuendena na mfumo wa kidijiti kwa lengo la kukuza uwajibikaji ,uwazi na ushirikiano kati ya wadau wa elimu kwa kutumia mfumo wa pamoja wa taarifa.
Kwa upande wake Uthibiti Ubora wa Shule Halmashauri ya Wilaya ya Buchosa Bi.Tunu M.Sarungi ameeleza na kufafanua kwamba mafunzo hayo ambayo yameandaliwa kwa lengo la kuwajengea uwezo Maafisa elimu kata, Wakuu wa shule wa Sekondari na Msingi pamoja na wenyeviti wa timu za uthibiti ubora wa shule za ndani kutumia mfumo wa kisasa kwa ufanisi katika kusimamia na kufuatilia viwango vya ubora wa elimu utawasaidia katika maeneo yao ya kazi.
Aidha mafunzo hayo ya mfumo wa kidijiti yanatarajia kuwajengea uwezo jumla ya washiriki 297 Maafisa elimu kata 21, Wakuu wa sekondari na Msingi 138 na wenyeviti wat imu za ndani 138.Hata hivyo mafunzo hayo ya kidijiti yatafanyika kwa awamu 4 kuanzia tarehe 15 hadi 18 Julai 2025.
Sambamba na hayo mafunzo ya mfumo wa Kidijiti yamejikita katika kutoa uelewa wa kina kwa washiriki kuhusu matumizi ya mfumo wa kidijiti wa uthibiti ubora wa shule ili kila mshiriki afahamu majukumu yake namna ya kuyatekeleza.
Buchosa District Council
Anuani: 44 Buchosa - SENGEREMA
Simu: 0759941297
Simu ya kiganjani: 0765029662
Barua pepe: ded@buchosadc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Hamlashauri ya Wilaya ya Buchosa. Haki zote zimehifadhiwa