Kongomano la maandalizi ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 Wananchi watoa maoni yao katika nyanja tofauti ikiwemo Utawala Bora,Uchumi imara,Amani,Utulivu na Umoja katika Halmashauri ya Wilaya ya Buchosa Mkoani Mwanza.
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeanza kuratibu maandalizi ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050. Serikali inatambua kuwa, maono na maratajio ya watanzania na mbinu za kuyafikia zinatokana na watanzania wenyewe kupitia ushirikishwaji madhubuti katika maandalizi na utekelezaji wa mipango ya maendeleo.
Kongomano hilo ambalo limefanyika tarehe 09, Agosti, 2024 katika ukumbi wa Shule ya Sekondari Nyehunge mbele ya mgeni rasmi Katibu Tawala wa Wilaya ya Sengerema Bw.Cuthbert Midala ambaye alimwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Sengerema, ambapo alioongoza Mdahalo kwa kupata maoni ya wadau mbalimbali pamoja na wananchi katika maandalizi ya Dira ya Taifa ya Maendeleo kuelekea 2050.
Bw.Midala ameeleza na kufafanua kwamba lengo la Kongamano hilo ni kuchukua maoni ya wananchi juu ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 katika nyanja tofauti, ikiwa ni pamoja na Utawala bora,Ujasirimali,Ulinzi na Usalama,ajira na Sekta ya Kilimo Ufugaji na Uvuvi na maoni hayo yataenda kuchakatwa na kuandaa Dira mpya ambayo itahakikisha inafikia malengo,nia na shauku ya wananchi katika miaka 25 inayokuja.
Aidha Katibu Tawala wa Wilaya ya Sengerema amesema kwamba Mikakati ya Serikali ni kupanga namna ya kutekeleza maoni hayo kupitia Taasisi na Sekta mbalimbali zinazosimamia maoni ya wananchi yanatolewa na hivyo, kuwataka wananchi waendelee kutoa maoni yao kupitia njia ya mtandao ambapo wanaweza kutoa maoni mbalimbali kwa kubonyeza *152*00# baada hapo unabonyeza namba 8 baada hapo unabonyeza namba 4 na kutoa maoni.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Buchosa Bw.Deogratius Lihengelimo ameeleza kuwa ili kufikia malengo ya Dira 2050 Serikali imeweka jitihada ya kuandaa Dira mpya ya Maendeleo ya Taifa ambayo itakwenda mpaka 2050 kwa kuwashirikisha wadau mbalimbali pamoja wananchi kuchukua maoni yao wanapendekeza nini katika Tanzania waitakayo kufikia 2050.
Vilevile ametoa shukrani za pekee kwa wananchi ambao walijitokeza kutoa maoni yao kuelekea Dira mpya ya Maendeleo ya Taifa 2050 ambapo wananchi waliweza kutoa maoni yao juu ya fursa mbalimbali ambazo zinapatikana katika Halmashauri ya Wilaya ya Buchosa kama Sekta ya kilimo,Ufugaji na masuala ya Uvuvi na kwamba kuna umuhimu kuanzishwa kwa viwanda ambavyo vitawezesha kuchakata malighafi na pia kuwepo kwa masoko ya uhakika kwa wakulima.
Naye Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Mipango Kampasi ya Mwanza Dkt. Fredrick A.Mfinanga ambaye alialikwa kama mwezeshaji katika Kongamano hilo alifafanua kwamba katika Dira ya Maendeleo ya Taifa ya 2025 Serikali imeweza kuwekeza katika miundombinu ya barabara,Sekta ya Afya,Kilimo,hata hivyo amesisitiza kuelekea Dira mpya ya Maendeleo ya Taifa 2050 Serikali iboreshe zaidi katika maeneo ya Kilimo ili iweze kutoa ajira nyingi kwa Vijana sambamba na kuongeza tija katika kuzalisha na kutafuta masoko ya uhakika ya bidhaa ambazo watazalisha na kuandaa viwanda ambavyo vitaanzia vijijini kwa ajili ya kuchakata malighafi.
Katibu Tawala wa Wilaya ya Sengerema Bw.Cuthbert Midala akiongoza Mdahalo katika Kongomano la maandalizi ya Dira ya Taifa ya Maendeleo ya 2050 ambalo limefanyika katika ukumbi Shule ya Sekondari ya Nyehunge siku ya Ijumaa tarehe 09/08/2024 ambapo wananchi waliweza kutoa maoni yao.
Baadhi ya Wananchi,Viongozi wa Vyama vya Siasa,Asasi za kiraia,Wazee wa Kimila,wafanyabiashara,Wanafunzi pamoja wadau mbalimbali walijokeza na kutoa maoni katika Kongamano la maandalizi ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 ambalo lilifanyika katika ukumbi wa Shule ya Sekondari Nyehunge tarehe 09,08,2024.
Buchosa District Council
Anuani: 44 Buchosa - SENGEREMA
Simu: 0759941297
Simu ya kiganjani: 0765029662
Barua pepe: ded@buchosadc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Hamlashauri ya Wilaya ya Buchosa. Haki zote zimehifadhiwa