KAMPENI YA MSAADA WA KISHERIA YA MAMA SAMIA
Wananchi wa Kijiji cha Itumbuli wapatiwa elimu ya msaada wa kisheria kupitia Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia Katika Halmashauri ya Wilaya ya Buchosa.
Elimu hiyo imetolewa leo tarehe 22, Februari, 2025 katika Kijiji cha Itumbuli katika Kata ya Nyakaliro ambapo wananchi wameweza kupatiwa elimu ya kisheria katika masula mbalimbali ya ukatili wa kijinsia,migogoro ya ardhi,mirathi,Matunzo ya Watoto,migogoro ya ndoa,madai,jinai,mfuko wa Tasaf,cheti cha kuzaliwa,uvunjifu wa utawala bora na haki za binadamu.
Akizungumza wakati wa zoezi hilo Msajiri Msaidizi wa watoa huduma ndogo za kisheria wa Halmashauri ya Buchosa Bw.Florian Mkangala ameeleza na kufafanua kwamba wananchi watakiwa kutumia fursa hiyo adhimu kwa kutoa malalalamiko na kero walizonazo ili yaweze kupatiwa ufumbuzi na watoa huduma za kisheria.
Ameongeza kuwa zoezi hilo la Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia katika Halmashauri ya Wilaya ya Buchosa litadumu kwa siku tisa pekee ambapo zoezi hili litamalizika tarehe 27, Februari,2025 na kuwataka wananchi kuendelea kujitokeza kwa wingi ili waweze kutumia fursa hiyo muhimu.
Lengo la Kampeni hii ni kulinda na kukuza upatikanaji wa haki kwa wote kupitia huduma ya msaada wa kisheria nchini.
Buchosa District Council
Anuani: 44 Buchosa - SENGEREMA
Simu: 0759941297
Simu ya kiganjani: 0765029662
Barua pepe: ded@buchosadc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Hamlashauri ya Wilaya ya Buchosa. Haki zote zimehifadhiwa