Shirika la ABC Impact kwa ushirikianona wa Mainsprings, watoa baiskeli 150 kwa wananchi wenye mazingira magumu ili kuwawezesha kuleta mabadiliko katika familia, kukabiliana na changamoto za masafa marefu katika Halmashauri ya Wilaya ya Buchosa.
Tukio hilo limefanyika leo Februari,06,2025 katika Shule ya English Medium ya Joseph and Marry Kijiji cha Kahunda Kata ya Katwe ambapo Mgeni rasmi alikuwa Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Buchosa Bw.Masalu Kaswa ambaye pia ni Afisa Maendeleo wa Halmashauri ya Buchosa amewataka walengwa hao kuzitumia baiskeli hizo kwa matumizi sahihi ili ziweze kuwa kwamua kwenye changamoto ya usafiri.
Aidha Bw.Kaswa amewataka wazazi na walezi kujituma na kuacha tabia ya kuwa tegemezi na badala yake kuendeleza ujuzi wa watoto wao wanaopata katika shule hiyo ikiwa pamoja na ujuzi wa shughuli za kilimo.
“Watoto wetu wanafundishwa hapa vitu vizuri kwa hivyo tujitahidi tusije tukasema kwamba wataendelea kusaidia misaada,misaada huwa ina mwisho”Amesisitiza Bw.Kaswa.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Ufuatiliaji na Tathmini wa Shirika la Mainsprings Bw. Sebastian Pius ameeleza na kufafanua kwamba wamejikita katika kutoa elimu ya mageuzi,kusaidia watoto wanaotoka katika mazingira magumu,huduma ya afya kupitia zahanati zinazopatikana katika vituo pamoja na kutoa elimu ya kilimo endelevu ambapo kilimo hicho hakitumii mbolea za dukani wala dawa za dukani.
Bw.Pius ameeleza kwamba wanatoa matibabu bure kwa watoto na wananchi ambao ni walengwa wa mradi huo (wanamaendeleo) ambao wanaishi katika mazingira magumu pamoja na kutoa pembejeo za kilimo ikiwemo mbegu, majembe ya kulimia na keni kwa ajili ya umwagiliaji ikiwa lengo ni kuwawezesha kupiga hatua katika maisha yao ya kila siku.
“ Mpango mkakati wa Mainsprings ni kusaidia wanamaendeleo katika mahitaji manne muhimu ya jamii za vijijini: elimu, hifadhi, huduma za afya na kilimo cha kudumu.”Amesema Bw.Pius.
Naye Meneja wa Shirika lisilo la Kiserikali la ABC Impact Bw.Mohammed Musa amesema kwamba kazi kubwa ya Shirika hilo limejikita kusaidia wananchi wanaoishi katika mazingira magumu kwa kutoa usafiri wa baiskeli.
Pia wanapogramu inayoitwa Back to school ambayo lengo lake ni kugawa baiskeli kwa wanafunzi ili kupunguza vishawishi,mimba ambavyo wanaweza kupata kwa baadhi ya bodaboda ambao sio waadilifu pindi wanapoomba msaada wa usafiri pamoja kutatua changamoto ya usafiri kwa wanafunzi hao ambapo kwa wanafunzi wakike wanapewa kwa asilimia 90 na kwa wavula kwa asilimia 10.
Hata hivyo kupitia mpango wa Bikes for Changemakers wameweza kukagwa baiskeli 150 kwa walengwa 62 ambapo kila familia imepata baiskeli mbili na pamoja kila mtoto ambapo itasaidia katika matumizi mbalimbali ikiwa watoto kutumia kwenda shule, na wazazi kuhudhuria kwenye shughuli za kiuchumi, kanisani,msikitini na sehemu mbalimbali ili kupunguza changamoto ya usafiri kwa wakazi hao.
Pendo Mtakubwa ni Mkazi wa Kijiji cha Kahunda ambaye ni mwanamaendeleo kwa muda miaka mitatu sasa ametoa shukrani za dhati kwa Mashirika hayo wawili Shirika la Mainsprings na ABC Impact kupitia Serikali kwa kuwaletea usafiri wa baiskeli ambapo utasaidia kutatua changamoto ya usafiri.
Buchosa District Council
Anuani: 44 Buchosa - SENGEREMA
Simu: 0759941297
Simu ya kiganjani: 0765029662
Barua pepe: ded@buchosadc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Hamlashauri ya Wilaya ya Buchosa. Haki zote zimehifadhiwa