Mbunge wa Jimbo la Buchosa Mhe.Erick Shigongo amefanya Hafla fupi ya kukabidhi gari la kubeba wagonjwa kwa wananchi wa Kisiwa cha Kome chenye jumla ya Kata nne Kata ya Buhama,Lugata,Bugoro na Nyakasasa.
Akizungumza na Wananchi wa Kisiwa hicho jana tarehe 03, Januari,2025 Mhe.Shigongo ameishukuru Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Mhe.Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwapatia Wananchi gari jipya la kubebea wagonjwa lenye usajili wa STN 3630 ambapo gari hilo lisaidia kupunguza kero na changamoto ya kusafirisha wagonjwa pindi watakapokuwa wanahitaji rufaa kwenda Hospitali ya Wilaya au Hospitali ya Kanda Bugando Mwanza.
Aidha Mhe.Shigongo ametoa wito kwa Wananchi wa Jimbo la Buchosa kuendelea kumwombea na kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kazi nzuri anayoifanya ya kuleta Maendeleo katika Jimbo la Buchosa.
“Nataka nikumbukwe na watu kwa kuwaletea Wananchi Maendeleo”Amesema Mhe.Erick Shigongo Mbunge wa Jimbo la Buchosa.
Katika hatua nyingine Mbunge wa Jimbo la Buchosa Mhe.Erick Shigongo amefanya ziara ya kutembelea na kukagua mradi wa ujenzi wa Shule mpya ya Sekondari Bugoro iliyopo Kata ya Bugoro ambapo ameridhishwa na hatua za ujenzi wa Shule hiyo.
Wananchi wa Kisiwa cha Kome wamemetoa shukurani za dhati kwa Serikali ya Awamu ya sita kwa kupatiwa gari jipya la wagonjwa ambapo litapunguza kadhia iliyokuwa ikiwakumba hasa kwa kina mama wajawazito.
Hafla hiyo ya kukabidhi gari la Wagonjwa kwa Kisiwa cha Kome imefanyika Kijiji cha Nyamiswi katika Kata ya Buhama.
Buchosa District Council
Anuani: 44 Buchosa - SENGEREMA
Simu: 0759941297
Simu ya kiganjani: 0765029662
Barua pepe: ded@buchosadc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Hamlashauri ya Wilaya ya Buchosa. Haki zote zimehifadhiwa