Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongela, leo tarehe 05 Mei 2017 ameshiliki katika zoezi la ufyekaji na uteketezaji wa bangi katika Hifadhi ya msitu wa Buhindi katika kijiji cha Ilyamchele kata ya Kazunzu Wilayani Sengerema.
Katika uteketezaji huo Mkuu wa Wilaya ya Sengerema Emmanuel Kipole amemueleza mkuu waMkoa wa Mwanza John Mongela kuwa Wilaya ya Sengerema imejipanga katika maeneomanne katika kutokomeza matumizi ya bangi pamoja na madawa mengine ya kulevya.
“Mheshimiwa mkuu wa Mkoa tumejipanga kutokomeza kadhia hii katika maeneo manne, maeneo hayo niuzalisha, usafirishaji, uuzaji na utumiaji” amesemaKipole.
Uteketezajihuo wa bangi umehusisaha watumishi wa ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Buchosa, watumishi wa Hifahi ya msitu Buhindi pamoja na vikosi mbalimbali vya Ulinzi na Usalama vya Mkoa wa mwanza.
Akizungumza baada ya uteketezaji wa Bangi Mkuu wa mkoa John Mongela amemuagiza mkuu waWilaya ya Sengerema Emmanuel Kipole kuhakikisha mifugo yote iliyomo kwenyehifadhi hiyo inatolewa na kutoruhusu shughuli za kibinadamu ndani ya msitu huo kufanyika.
Pia mkuu wa Mkoa John Mongela amewashukuru raia wema wanaoendelea kutoa taarifa za uhalifu na kuwezesha kuzuia kwa matendo ya uovu katika maeneo yao.
“niwapongeze sana wananchi watoataarifa” ameseaMongela.
Zoezila uteketezaji na ufyekaji bangi limefanyika sanjari na agizo la Rais waJamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli ikiwa ni mapambanodhidi ya kutokomeza madawa ya kulevya nchi nzima.
Buchosa District Council
Anuani: 44 Buchosa - SENGEREMA
Simu: 0759941297
Simu ya kiganjani: 0765029662
Barua pepe: ded@buchosadc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Hamlashauri ya Wilaya ya Buchosa. Haki zote zimehifadhiwa