Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Dunstan Kitandula amewataka wananchi wa Kisiwa cha Maisome kifuata taratibu zilizowekawa na Serikali ili kulinda msitu wa asili wa Maisome usitoweke na kuleta athari za amabadiliko ya tabia nchi.
Kauli hiyo imetolewa jana Jumamosi 14,Septemba,2024 na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe.Dunstan Kitandula alipofanya ziara ya siku moja kwenye Kisiwa cha Maisome alipokuwa akizungumuza na wananchi juu ya adhima ya Serikali kuridhia ombi la wananchi wa kisiwa cha Maisome kupatiwa hekta 2,871.782 kwa ajili ya matumizi ya shughuli mbalimbali za kijamii.
"Msitu wa Maisome una hekata zaidi ya 12000 wananchi wamepewa hekta 2871 hivyo utabakiwa na Hekta 9319” amesema Naibu Waziri Kitandula.
Aidha Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii amesema Serikali imeweka taratibu za wananchi kuokota kuni kwa ajili ya kupikia kwenye hifadhi ya msitu huo hivyo jamii inatakiwa kufuata taratibu zilizoweka za kuokata kuni mara tatu kwa wiki kwa angalizo la kutokukata miti ambayo ipo ndani ya hifadhi hiyo.
Kwa upande wake Mbunge wa Buchosa Eric Shigingo alieza na kufafanua kwamba kiu ya wanabuchosa wa Kata ya Maisome nikuona wanapiganiwa katika suala zima la maendeleo.
Shigongo amesema ilikuwa ni ajenda yake ambayo alitaka ifike mwisho ili kila wananchi wa Buchosa aweze kunufaika na rasimali za nchi huku akiwataka wananchi kuendelea kukiunga mkono chama cha Mapinduzi ambayo sera yake ni kila mtanzania apate haki katika nchi hii.
"Nilisimamia ajenda hiyo Bungeni na Serikali imesikia kilio cha wananchi asante sana Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuwaona wananchi wa Kata ya Maisome Buchosa” amesisitiza” Shigongo.
Naye Bakari Mohamed Meneja TFS Kanda ya Ziwa amefafanua kwamba wamepokea maelekezo ya Serikali hivyo wanachosubiria na mchakato wa kishireia ukamilike ili wananchi wakabidhiwe maeneo waliyopewa na Serikali.
Lukomwa Maendeka ni mkazi wa kisiwa cha Maisome amesema wamekuwa na changamoto ya kukosa maeneo ya malisho ya mifugo hali iliyopelekea mifungo yao kwenda hifadhini ambapo wamekuwa wakitozwa faini kubwa kati ya Shilingi 50,000 hadi Shilingi 100,000 pindi mifugo inapoingia hifadhini hapo na kupelekea baadhi ya wananchi kuuza mifugo yao.
Naibu Waziri wa Maliasli na Utalii Mhe.Dunstan Kitandula akiwasili katika Kisiwa cha Maisome na kupokelewa na mwenyeji wake Mbunge wa Jimbo la Buchosa Mhe.Eric Shigongo mapema jana wakati wa ziara ya kutembelea hifadhi katika Kisiwa cha Maisome na kuongea wananchi.
Buchosa District Council
Anuani: 44 Buchosa - SENGEREMA
Simu: 0759941297
Simu ya kiganjani: 0765029662
Barua pepe: ded@buchosadc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Hamlashauri ya Wilaya ya Buchosa. Haki zote zimehifadhiwa