Katibu Tawala Mkoa wa Mwanza Ndugu Balandya Elikana amewataka watendaji kuendelea kusimamia Miradi ya Maendeleo kwa uadilifu mkubwa kwa kushiriakiana na wataalamu kwa munufaa ya wananchi na Taifa kwa ujumla.
Katibu tawala ametoa maelekezo hayo leo tarehe 18 Juni, 2025 katika ukumbi mkubwa wa Halmashauri wakati akiongoza baraza maalum la hoja za mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali kwa halmashauri Buchosa katika mwaka wa fedha unaoishia Juni 30, 2024.
Balandya ameeleza na kufafanua kwamba Serikali inafanya kazi kubwa katika kuboresha maisha ya wananchi, kila mtumishi akatimize wajibu kwa kuhakikisha dhamana aliyopewa anaitendea haki kwa kufanya kazi kwa bidii.
Aidha Bandaya ameitaka halmashauri kuendelea kulipa madeni ya wazabuni na kuwasilisha madeni ya watumishi ili kuondoa hoja ya madeni ya wazabuni pamoja na watumishi katika Halmashauri ya Buchosa.
Hata hivyo Mkaguzi Mkuu wa nje wa Hesabu za Serikali Mkoa wa Mwanza CPA. Richson Ringo amesema kwa hesabu za mwaka wa fedha 2023/24 halmashauri ya wilaya ya Buchosa imepata hati safi na imekua ikipata hati hizo kwa miaka mitatu mfululizo.
Sambamba na hilo ametanabaisha kuwa kwa mwaka 2023/24 baada ya ukaguzi kulikua na jumla ya mapendekezo 30 ambapo hoja 20 zimefungwa na 9 zipo katika hatua mbalimbali na hoja moja bado haijafanyiwa kazi.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya Buchosa Mhe.Idama Kibanzi ametoa shukrani za pekee kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutoa fedha kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo katika Halmashauri ya Buchosa.
Buchosa District Council
Anuani: 44 Buchosa - SENGEREMA
Simu: 0759941297
Simu ya kiganjani: 0765029662
Barua pepe: ded@buchosadc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Hamlashauri ya Wilaya ya Buchosa. Haki zote zimehifadhiwa