Katibu Tawala Mkoa wa Mwanza awataka wananchi kutunza na kulinda miundombinu mbalimbali ambayo Serikali inatumia fedha nyingi katika kutekeleza miradi ya Maendeleo katika Halmashauri ya Wilaya ya Buchosa Mkoani Mwanza.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza Bw.Elikana Bulandya ameyasema hayo tarehe 13, Septemba, 2024 wakati wa ziara yake ya kutembelea na kukagua miradi akiwa katika Kituo cha Afya Nyakasungwa ambapo ameeleza na kufafanua kwamba wananchi wanao wajibu wa kutunza miundombinu ya ujenzi wa miradi katika maeneo yao yanayowazunguka kwani Serikali inatoa fedha nyingi kujenga miradi hiyo ya maendeleo ili wananchi waweze kunufaika na kupata hudama bora na kwa wakati.
Aidha Bw.Bulandya ameeleza kufafanua kwamba mradi wa ujenzi wa Kituo cha Afya cha Nyakasungwa ambacho kimejengwa kwa Mapato ya ndani ya Halmashauri kitakapokamilika kitaboresha huduma za afya kwa wananchi na kupunguza vifo vya watoto chini cha wa miaka 5,kupunguza vifo vya kinamama wajawazito na kitasaidia kupunguza umbali mrefu kwa wananchi kufuata huduma.
Katika hatua nyingine Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza ametembelea na kujionea hatua wa Ujenzi wa Vyumba viwili vya madarasa pamoja na matundu sita ya vyoo katika Shule ya Msingi Nyehunge iliyopo Kata ya Nyehunge, sambamba na miiradi mingine ambayo ni Ujenzi wa Mradi wa umwagiliaji Sukuma uliopo kijiji cha Sukuma Kata ya Bukokwa,Mradi wa Vijana (Toroka uje) uliopo Kata ya Nyakalilo na Mradi wa tenki la maji Nyakalilo.
Hata hivyo Katibu Tawala wa Mwanza ametoa maelekezo kwa Mkuu wa Wilaya ya Sengerema kuwa Miradi yote ambayo itatembelewa na Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2024 kuwepo na nyaraka mbalimbali muhimu za miradi zikiwa zimepangwa vizuri sambamba na kukamilisha mapungufu ambayo yamejitokeza wakati wa ukaguzi wa miradi hiyo.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Sengerema Mhe.Senyi Ngaga ameeleza kwamba ameyapokea maelekezo hayo ya Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza na kuahidi kuyafanyia kazi ikiwa ni pamoja kuandaa nyaraka muhimu na kurekebisha kasoro ambazo zimejitokeza katika miradi hiyo.
Buchosa District Council
Anuani: 44 Buchosa - SENGEREMA
Simu: 0759941297
Simu ya kiganjani: 0765029662
Barua pepe: ded@buchosadc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Hamlashauri ya Wilaya ya Buchosa. Haki zote zimehifadhiwa