Katibu Tawala Mkoa wa Mwanza aridhishwa na Maadalizi ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika 27, Novemba,2024 nchi nzima.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza Bw.Elikana Bulandya ameyasema hayo leo tarehe 21, Novemba,, 2024 wakati wa ziara yake ya kutembelea,kukagua na kuangalia mwenendo wa maandalizi ya kuelekea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa ambao utakaofanyika tarehe 27,Novemba,2024 ambapo amekagua na kujiridhisha namna ya uandaji na mchakato mzima wa maandalizi unavyofanyika na kuagiza mamlaka husika inayosimamia zoezi la Uchaguzi kusimamia kikamilifu ili kuepusha malalamiko yasiyokuwa na ulazima wakati zoezi la uchaguzi linaendelea.
Aidha Bw.Bulandya ameeleza kufafanua kwamba kuelekea Uchaguzi wa Serikali za mitaa Viongozi wenye dhamana wahakikishe wanasimamia vyema zoezi la Uchaguzi ili uwe haki na usawa katika Halmashauri ya Wilaya ya Buchosa.
Katika hatua nyingine Bw.Bulandya ametembelea na kujionea Vituo kadhaa na maandalizi yake ambapo vitatumika wakati wa Uchaguzi wa Serikali Mitaa ambapo ameridhishwa na maadalizi hayo na kuwataka Viongozi ngazi ya Wilaya kuhakikisha vituo vinakuwa katika hali ya usafi na kuweka mazingira rafiki kwa watumiaji.
Kwa upande wake Katibu Tawala wa Wilaya ya Sengerema Bw.Cuthberth Midala akiongea kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Sengerema Mhe.Senyi Ngaga ameeleza kwamba hali ya kisiasa ipo katika hali ya usalama na maandalizi ya mchakato kuelekea Uchaguzi wa Serikali za mitaa unaendelea vizuri.
Naye Msimamizi wa Uchaguzi ngazi ya Wilaya Bw.Benson Mihayo ameeleza kwamba atahakikisha mchakato wa maandalizi unakamilika kwa wakati na vifaa vyote vya uchaguzi vitafika maeneo yote kwa muda uliopangwa katika vituo vyote vya kupigia kura.
“Serikali za Mitaa,Sauti ya Mwananchi Jitokeze Kushiriki Uchaguzi”.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza Bw.Elikana Bulandya alivaa kofia akikagua baadhi ya nyaraka mbalimbali na kujiridhisha kwa ajili ya Maandalizi kuelekea Uchaguzi wa Serikali za mitaa ambao utafanyika tarehe 27,Novemba,2024.
Buchosa District Council
Anuani: 44 Buchosa - SENGEREMA
Simu: 0759941297
Simu ya kiganjani: 0765029662
Barua pepe: ded@buchosadc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Hamlashauri ya Wilaya ya Buchosa. Haki zote zimehifadhiwa