Mwenyekiti wa UWT Taifa aridhishwa na kupongeza Miradi ya Maendeleo katika Halmashauri ya Wilaya ya Buchosa Mkoani Mwanza.
Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa Chama cha Wanawake wa Chama cha Mapinduzi Tanzania Bi.Mary Chatanda leo 06,Agosti,2024 ametembelea na kukagua Mradi wa Kituo cha Afya Nyakasungwa kilichopo Kata ya Nyakasungwa ambapo ameridhishwa na hatua ya ujenzi wa kituo hicho ambacho kimetumia fedha za mapato ya ndani.
Mwenyekiti wa UWT amempongeza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Buchosa Bw.Benson P.Mihayo kwa kusimamia kikamilifu ukusanyaji wa mapato kupelekea kujenga Kituo cha Afya Cha Nyakasungwa ambacho kipo katika hatua ya ukamilishaji ikiwa pamoja upakaji wa rangi,milango na madirisha.
“Tunawapongeza sana sana kwa kazi nzuri mnayofanya,hongereni sana,Nampongeza Mhe Diwani,Mkurugenzi Mtendaji kwa kusimamia kikamilifu ukusanyaji wa mapato”Amesisitiza Bi.Chatanda.
Aidha Bi.Chatanda amesema na kufafanua kwamba Serikali inatoa fedha nyingi kwa ajili ya kuleta Miradi ya Maendeleo ikiwemo miradi ya afya ili wananchi waweze kupata huduma bora na kwa wakati.
Kwa upande Mkuu wa Wilaya ya Sengerema Mhe.Senyi Ngaga akiongea na wananchi wa Kijiji cha Luchili Kata ya Nyazenda amefafanua kwamba Serikali ya awamu ya sita imekuwa ikitekeleza miradi mingi ya Maendeleo hususani kwenye Sekta ya afya, Elimu,Maji na Miundombinu ya barabara ambapo amesema barabara ya kutoka Sengerema kwenda Nyehunge itakuwa kwenye kiwango cha lami.
“Najua hilo ni hitaji kubwa la wanabuchosa wote kwa sababu inatuanganisha” Amesema Mkuu wa Wilaya ya Sengerema.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Buchosa amesema kwamba kupitia Waheshimiwa Madiwani pamoja menejimenti na watumishi kwa ujumla wake wanashirikiana kuhakikisha mapato yanapatikana na kutumika kwa usahihi sambamba na kutoa motisha kwa watumishi ambao wanafakazi kwa bidii na uadilifu katika Halmasahauri ya Wilaya ya Buchosa.
Hata hivyo,Halmashauri ya Wilaya ya Buchosa ilitenga fedha kiasi cha shilingi 150,000,000/= kwa mwaka wa fedha 2023/2024 kutoka fedha mapato ya ndani kwa ajili ya kuanza ujenzi wa miundombinu ya kituo cha Afya katika Kata ya Nyakasungwa kwa kutekeleza ujenzi wa jengo la wagonjwa wa nje (OPD) ambapo ujenzi unatarajiwa kukamilika mwezi 8 mwaka huu,mpaka sasa fedha iliyotumika ni shilingi 83,648,040/=.
Wananchi wa Kijiji cha Luchili na maeneo jirani wamejitokeza kwa wingi kwenye ziara ya Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Taifa Bi.Mary Chatanda leo,ambapo amewataka kujitokeza kushiri kwenye Uchaguzi wa Serikali za Mitaa na kuwachagua Viongozi wanaowataka.
Mwonekano wa jengo la Kituo cha Afya Nyakasungwa ambapo mpaka sasa umegharimu kiasi cha fedha shilingi 83,648,040/= kitakapokamilika kitasaidia kutoa huduma kwa wananchi wa Nyakasungwa na maeneo jirani.
Buchosa District Council
Anuani: 44 Buchosa - SENGEREMA
Simu: 0759941297
Simu ya kiganjani: 0765029662
Barua pepe: ded@buchosadc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Hamlashauri ya Wilaya ya Buchosa. Haki zote zimehifadhiwa