Mkutano Mkuu wa Mwaka wa jukwaala Mashirika Yasiyo ya Kiserikali (NGOs) watoa Tathmini ya Mchango kwa kipindi cha Miaka mitano katika Wilaya ya Sengerema.
Mkutano huo umefanyika tarehe 26,Juni,2025 katika ukumbi wa mikutano Halmashauri ya Sengerema ambapo umewakutanisha wawakilishi kutoka mashirika mbalimbali yasiyo ya kiserikali ambayo yanayotekeleza shughuli za kuwahudumia wananchi katika Wilaya ya Sengerema ambayo ina Halmashauri ya Buchosa na Halmashauri ya Sengerema kwa lengo la kujadili tathmini ya utekelezaji wa shughuli za maendeleo, changamoto zilizopo, mafanikio yaliyopatikana na kuweka mikakati ya pamoja ya kuboresha huduma kwa jamii.
Afisa Maendeleo ya Jamii wa Halmashauri ya Buchosa Bw.Alto Mbikiye akimwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Sengerema Mhe.Senyi Ngaga ameeleza na kufafanua kwamba Mashirika yasiyo ya kiserikali kushirikana kwa pamoja na Serikali katika kuwaletea wananchi maendeleo katika Sekta mbalimbali hapa nchini.
Aidha wawakilishi kutoka Mashirika yasiyo ya kiserikali wakiwasilisha taarifa zao tathmini za michango ya mafanikio katika jamii kwa kipindi cha miaka 5 kwa nyakati tofauti wamweza kueleza walivyowezeza kutoa michango yao katika sekta ya Afya,elimu na Kilimo na Ufugaji,Uwezeshaji kiuchumi pamoja na kuongeza uelewa wa wananchi kuhusu haki zao na kushiriki katika mchakato wa utawala bora.
Kwa upande wa Asasi za Kiraia wameiomba Serikali kuimarishwa kwa mtandao wa NGO ili kusaidia mtao wa NGO kupata Ofisi ,rasilimali na mafunzo ili uimarike kiutendaji,kuwepo kwa mkutano wa Mwaka wa NGOs na Serikali ili kujadili mafanikio,changamoto na kuweka mikakati ya pamoja ya maendeleo,sambamba na hilo wameomba Serikali kuanzishwa kwa mfumo wa kutambua na kutunza taarifa za NGOs ambapo itasaidia katika upangaji wa maendeleo kwa ushirikiano.
Hata hivyo mkutano huo ambao umebeba dhamira ya kuimarisha mshikamano baina ya wadau wa maendeleo na kuhakikisha rasilimali zinatumika kwa tija kwa manufaa ya wananchi katika Wilaya ya Sengerema.
Kikao hicho kimebeba kaulimbiu inayosema “Tathmini ya mchango wa Mashirika yasiyo ya kiserikali katika maendeleo ya taifa 2020/2021 – 2024 /2025”.
Buchosa District Council
Anuani: 44 Buchosa - SENGEREMA
Simu: 0759941297
Simu ya kiganjani: 0765029662
Barua pepe: ded@buchosadc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Hamlashauri ya Wilaya ya Buchosa. Haki zote zimehifadhiwa