Mkuu wa Wilaya ya Sengerema Emmanuel Kipole amekabidhi magari mawili ya wagonjwa ya shilingi milioni 300 yalitolewa na serikali kwa lengo la kusaidia huduma za afya za mama na mtoto katika halimashauri za sengerema na Buchosa na kuwatka wakurugenzi wayatunze magari hayo na yafanyekazi iliyokusudiwa.
Akikabidhi magari hayo kwa wakurugenzi wa halimashauri za Buchosa na Sengerema zinazounda Wilaya ya Sengerema alisema serikali ya awamu ya tano imejikita kusaidia wananchi na kusogeza hudama kwa wananchi hasa wa vijijini ambao hupoteza maisha kutokana na kutokuwepo kwa usafiri katika maeneo yao hivyo imetoa magari hayo ili yawasadie wananchi hao.
Alisema kuwa hata mvumila mtu yoyote au kiongozi yoyote atakaye tumia gari hayo kwa shughuri zake binafsi kwa kubeba kitu chochote kinyume na mgonjwa atachukuliwa hatua za kisheria hivyo wanapaswa kuwa makini na matumizi ya magari li yawasaidie wagonjwa.
Kipole alisema kila mmoja anapaswa kutimiza wajibu wake kwa kutunza mali zinazotolewa na serikali kwa lengo la kusaidia wananchi magri haya yakakae katika vito vya afya yalikopangiwa Halimashauri ya Buchosa ni Kituo cha afya cha Kakobe Halimashauri ya Sengerema ni kituo cha Afya cha Kagunga .
Sambamaba na hayo kipole alisema kuwa Serikali imetoa zaidi ya milioni 600 za kujenga Haspitari ya Halimashauri ya Buchosa ili kusogeza huduma kwa wananchi fedha hizo zipo na ujenzi huo utaanza mara moja hivyo na kuwahisi wananchi waendelee kuiamini serikali yao kuwa inawajili na kuwadhamini.
Mkurugenzi wa halimashauri ya Sengerema Magesa Mafuru alisema kuwa magari haya yatasaidia wananchi wetu kuwahishwa kwenye vituo vya afya ili wapate matibabu na kuahidi kuyatunza vema ili yadumu kwa muda mrefu.
Buchosa District Council
Anuani: 44 Buchosa - SENGEREMA
Simu: 0759941297
Simu ya kiganjani: 0765029662
Barua pepe: ded@buchosadc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Hamlashauri ya Wilaya ya Buchosa. Haki zote zimehifadhiwa