Katibu Tawala wa Wilaya ya Sengerema ameongooza ziara ya kutembelea na kukagua miradi ya Maendeleo ambayo inapitiwa na mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2025 kwa ajili kufuatilia mafanikio na changamoto zilizopo ili kuhakikisha Mwenge unapokelewa vizuri katika Halmashauri ya Buchosa.
Katibu Tawala wa Wilaya ya Sengerema Bw.Cuthbert Midala akimwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Sengerema Mhe.Senyi Ngaga amesema miradi yote inayopitiwa na Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2025 katika maeneo yote, Wataalamu na Watendaji wahakikishe mapungufu yote ya miradi inayojengwa yafanyiwe kazi na kuzingatia ubora wa viwango na kuendana na thamani halisi ya fedha zilizotumika, na wahusika wote wawajibike kikamilifu katika jukumu hilo la kitaifa.
Ziara hiyo imefanyika leo tarehe 12/06/2025 kwa lengo la kuona maendeleo na ukamilishwaji wa Miradi hiyo. Miradi iliyotembelewa ni pamoja na Ujenzi wa nyumba ya mtumishi katika Zahanati ya Igwanzozu,jenzi wa vibanda vya soko Kata ya Bukokwa,Ufugaji wa Samaki Kata ya Kazunzu,Mradi wa maji Kata ya Bulyaheke , na Ujenzi wa shule Sekondari Chema Kata ya Bupandwa.
Kaulimbiu: “JITOKEZE KUSHIRIKI UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2025 KWA AMANI NA UTULIVU”
Buchosa District Council
Anuani: 44 Buchosa - SENGEREMA
Simu: 0759941297
Simu ya kiganjani: 0765029662
Barua pepe: ded@buchosadc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Hamlashauri ya Wilaya ya Buchosa. Haki zote zimehifadhiwa