Kamati ya Siasa CCM Wilaya ya Sengerema yaridhishwa na kupongeza utekelezaji wa Miradi ya sekta ya Afya na Miundombinu ya ujenzi wa VETA inayoendelea kutekelezwa katika Halmashauri ya Buchosa Mkoani Mwanza.
Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe, Rais,Dkt. Samia Suluhu Hassan katika juhudi za kuboresha na kukuza Uchumi wa Wananchi imeendelea kuleta neema katika sekta ya Elimu, Maji na miundombinu ya barabara kwa kutoa fedha za kujenga miradi na hatua za ukamilishaji zinaendelea vizuri.
Kamati ya Siasa Wilaya ya Sengerema CCM ikiongozwa na Mwenyeki wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya Mhe.Marco Makoye (DM) tarehe 03.Februari,2025 imetembelea na Kukagua Kituo cha Afya Lushamba ambacho kina jumla ya majengo Matano (5) Jengo la wagonjwa wanje (OPD),Jengo la Maabara,Jengo la Mama na mtoto,jengo la Upasuaji,na nyumba moja ya familia mbili, na kuonyeshwa kuridhishwa na ujenzi wa Kituo hicho ambacho kimegharimu shilingi 648,364,940.70 fedha kutoka Serikali kuu kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii TASAF,ambapo Kituo hicho hapo awali kilijulikana kama Zahanati ya Lushamba,kilianza kutoa huduma rasmi kama Kituo cha Afya mnamo Januari 2024.
Wakati huo huo, Wajumbe wa Kamati ya Siasa Wilaya ya Sengerema pia wamekagua ujenzi wa Chuo cha Ufundi VETA kinachojengwa kwa fedha kutoka Serikali Kuu katika Kijiji cha Kayenze Kata ya Nyehunge Halmashauri ya Buchosa, Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Sengerema Mhe,Makoye (DM) amesema kwamba Miradi ya Maendeleo inatakiwa kukamilika kwa wakati ili wananchi waweze kunufaika Miradi hiyo katika Halmashauri ya Buchosa.
Aidha Kamati hiyo ilipata wasaa wa kutembelea wagonjwa ambao walikuwa wanapatiwa huduma ya matibabu katika Kituo hicho na kupatiwa pole kama motisha kwa wagonjwa hao, sambamba na kusherekea miaka 48 ya Chama cha Mapinduzi kwa vitendo ambapo miti kadhaa ilipandwa kama kumbukumbu katika eneo la kituo hicho.
Kwa Upande wake Kaimu Mkurugenzi Mtendai wa Halmashauri ya Wilaya ya Buchosa Dkt.David Mndeba ambaye pia ni Mganga Mkuu wa Halmasahuri ya Buchosa ameeleza na kufafanua kwamba Serikali ya awamu ya Sita imetoa fedha kiasi cha shilingi 300,000,000/=kwa ajili ya kununua vifaa tiba mbalimbali kutoka bohari ya dawa (MSD) kununuliwa kwa vifaa tiba vimesaidia kuboresha huduma mbalimbali kama ultrasound (uchunguzi kwa njia ya kioo) na huduma za upasuaji.
Hata hivyo Dkt Mndeba ameongeza kuwa walifanikiwa kupokea vifaa mbalimbali kutoka Global Fund vikiwemo Vitanda 15, Magodoro 15, mashuka 60 na meza za kwenye vitanda hivyo.
Sambamba na hayo ameishukuru Kamati ya Siasa ya Wilaya ya Sengerema kwa kufanya ziara na kukagua maendeleo ya miradi katika Sekta ya Afya na kuwaomba waendelee kufanya ufuatiliaji huo ili kuwezesha miradi hiyo kukamilika kwa wakati.
Buchosa District Council
Anuani: 44 Buchosa - SENGEREMA
Simu: 0759941297
Simu ya kiganjani: 0765029662
Barua pepe: ded@buchosadc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Hamlashauri ya Wilaya ya Buchosa. Haki zote zimehifadhiwa