Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Buchosa, Crispin Luanda kwa pamoja na Balozi wa Japani nchini Tanzania, Masaharu Yoshida watia saini mkataba wa kusaidia upanuzi wa soko la Nyakaliro.
Mkataba huo umesainiwa mbele ya Naibu spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Tulia Ackson pamoja na Mbunge wa Kigoma Mjini Mhe Zitto Kabwe.
Mkataba wa upanuzi wa soko la samaki Nyakaliro una jumla ya kiasi cha dola 103,258 za kimarekani ambazo ni sawa na milioni 224 za kitanzania.
Mkataba huo umesainiwa leo katika makazi ya Balozi wa Japani yaliyopo Masaki jiji Dar es Salaam.
Katika ziara hiyo Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Buchosa, Crispin Luanda aliambatana na Mwenyekiti wa Halmashuri, Mhe Joseph Kanyumi pamoja na wataalamu toka Halmashauri ya Wilaya ya Buchosa.
Kutoka kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Buchosa, Crispin Luanda, Mbunge wa Kigoma mjini Mhe Zitto Kabwe, Naibu Spika wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe Tulia Ackson pamoja na Balozi wa Japan nchini Tanzania, Mhe Masaharu Yoshida.
Buchosa District Council
Anuani: 44 Buchosa - SENGEREMA
Simu: 0759941297
Simu ya kiganjani: 0765029662
Barua pepe: ded@buchosadc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Hamlashauri ya Wilaya ya Buchosa. Haki zote zimehifadhiwa