Kituo cha Afya Kome usiku wa kuamkia usiku wa leo umefanya upasuaji wa kwanza wa mama mjamzito kwa kutoa mtoto tumboni baada ya uzazi wa njia ya kawaida kushindikana kutokana na uzazi pingamizi.
Hali ya mama (Janeth Lusato) pamoja na mwanaye aliyezaliwa akiwa na uzito wa Kilogramu 3.9 inaendelea vizuri.
Janeth Lusato anatokea kitongoji cha Nyalusenyi kijiji cha Nyakabanga ambapo alikuwa akipatiwa huduma za kliniki katika zahanati ya Lugata iliyopo kata ya Lugata katika Halmashauri ya Wilaya ya Buchosa.
Ikumbukwe tarehe 30/11/2019 Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mheshimiwa Ummy Mwalimu alitembelea kituo cha Afya Kome ambapo alipata wasaa wa kukagua chumba cha kutolea huduma za Upasuaji pamoja na kuzindua chumba cha kuhifadhia majokofu ya kuhifadhia chanjo yanayotumia nishati ya jua (umeme wa jua) kwenye Zahanati ya Nyakasungwa Halmashauri ya Wilaya ya Buchosa
Pia ikumbukwe serikali ilitoa kiasi cha fedha milioni mia nne (400,000,000) kwa ajili ya ukarabati wa majengo ya kituo cha Afya Kome pamoja na kupeleka vifaa tiba vyenye thamani ya milioni mia mbili na kumi na mbili (212,000,000).
Maboresho haya yamesaidia wananchi wa kisiwa cha Kome kutokuwa na uhitaji wa kuvuka maji kufata huduma Sengerema.
Buchosa District Council
Anuani: 44 Buchosa - SENGEREMA
Simu: 0759941297
Simu ya kiganjani: 0765029662
Barua pepe: ded@buchosadc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Hamlashauri ya Wilaya ya Buchosa. Haki zote zimehifadhiwa