Halmashauri ya Wilaya Buchosa imeendelea kujipatia Hati safi kwa Miaka miwili mfululizo, katika kipindi hiki cha Serikali ya Awamu ya sita, Pamoja na usimamizi thabiti wa ukusanyaji wa mapato. Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri Mhe.Maximillian Mkungu ambaye anakiri licha ya mafanikio waliyoyapata chini ya Uongozi wa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Buchosa Mhe.Idama Kibanzi yapo mambo ambayo hawezi kuyasahau yakiwemo yale ya kimaendeleo katika Halmashauri ya Wilaya Buchosa, ambayo kimsingi ni hatua kubwa kulinganisha na kipindi walipoingia katika madaraka hayo.
Akitaja baadhi ya mafanikio hayo Makamu Mwenyekiti ambaye pia ni Diwani Kata Katwe amesema kuwa Halmshauri hiyo imepata Hati safi kwa miaka miwili, ambapo amesisitiza kwamba ni Ushirikiano baina ya Viongozi Mkurugenzi Mtendaji ,wakuu wa idara na vitengo, Madiwani pamoja Mhe.Mbunge wa Jimbo la Buchosa.
“Kupata hati safi,siyo kwamba ni Waheshimiwa Madiwani tu,bali ni mshikamano uliopo ndani ya Halmashauri yetu,Waheshimiwa madiwani,Watumishi na Wananchi kwa ujumla ambao wanatuunga mkono katika shughuli za maendeleo” amesema Makamu Mwenyekiti Mhe.Mkungu.
Usimamizi na ufanikishaji wa miradi mikubwa ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa vyumba vya madarasa, miundombinu ya Barabara,Maji na huduma za afya, Usimamizi wa Mifuko mbalimbali ya Fedha, lakini kubwa zaidi likiwa ni suala la ukusanyaji mapato ndani ya Halmshauri kutoka katika vyanzo vya mapato.
Katika baraza hilo la Madiwani wageni waalikwa mbalimbali waliweza kuhudhuria ikiwa ni pamoja na Wakuu wa taasisi,Vyama vya siasa,viongozi wa dini,waandishi wa Habari na waatalamu kutoka makao makuu.
Buchosa District Council
Anuani: 44 Buchosa - SENGEREMA
Simu: 0759941297
Simu ya kiganjani: 0765029662
Barua pepe: ded@buchosadc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Hamlashauri ya Wilaya ya Buchosa. Haki zote zimehifadhiwa