Shirika la DWWT kupitia Mradi wa Imarisha jamii limefanikiwa kuwafikia wananchi kwa kutoa elimu ya jipime mwenyewe pamoja na kutoa mafunzo ya elimu ya matumizi ya dawa kinga katika Halmashauri ya Wilaya ya Buchosa.
Hayo yamesemwa na Afisa Tathmini na Ufuatiliaji Shirika la Dignity and Wellbeing for Women Living with HIV in Tanzania (DWWT) Bw. Elihuruma Laizer ambapo emeeleza na kufafanua kwamba kupitia Mradi wa Imarisha Jamii unaofadhiliwa na PEPFAR muda wa utekelezaji wa mradi huo ulikuwa ni wa mwaka mmoja ambapo ulianza mwezi Machi, 2023 na kumalizika Januari 2025 kwa kuhudumia Kata tatu ambazo ni Kata ya Bukokwa,Kasisa na Kata ya Bulyaheke katika Halmashauri ya Wilaya ya Buchosa.
Bw.Laizer amesema kwamba malengo ya makuu ya Mradi huo ni kuhakikisha wanatoa elimu ya matumizi ya kipimo cha jipime mwenyewe ambapo walilenga makundi hatarishi wakiwemo wavuvi,wasichana wadogo ambao wako kwenye rika la kubalehe na vijana pamoja na watu wengine ambao hawajapima na kutambua afya zao, na kutoa rai kwa wananchi kuendelea kujikinga na dhidi ya maambikizi ya virusi vya ugonjwa wa UKIMWI.
“Kupitia Mradi huu kwenye Kata tatu za Halmashauri ya Wilaya ya Buchosa tuliweza kuwafikia vijana kupitia mikutano ya kijamii,madangulo,pamoja na maeneo yenye mikusanyiko ya watu kama masoko kuwaelimisha na kuwapa vipimo vya jipime mwenyewe na kuhakikisha wanapima na kujua hali zao”. Amesema Bw.Laizer.
Aidha Bw. Laizer ameeleza kwamba waliwashirikisha Viongozi wa dini pamoja na wazee maarufu katika jamii kwa kufanya mikutano na kuwapa elimu ya uelewa juu ya huduma ambazo zinatolewa na Shirika la DWWT na matumizi sahihi ya dawa kinga na kutumia nafasi wazilizo nazo kuwaelimisha jamii wanazozihudumia kwa ufasaha pamoja na kuondokana dhana potofu ambayo imejengeka katika jamii juu ya maambukiza ya ugonjwa wa UKIMWI.
Hata hivyo Afisa Tathmini na Ufuatiliaji wa Shirika la DWWT ametoa shukrani za pekee kwa Halmashauri ya Wilaya ya Buchosa kwa kushirikiana kwa pamoja kufikisha huduma kwa wananchi hasa wavuvi katika maeneo mbalimbali,sambamba kuwashukuru wafadhili kutoka ubalozi wa Marekani PEPFAR kwa kuwazesha ruzuku ya kuweza kutekeleza Mradi wa mwaka mmoja ambapo lengo la mradi limefanikiwa kwa kiasi kikubwa.
Kwa upande wake Kaimu Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Wilaya ya Buchosa Bi. Trezia Kaole amelishukuru Shirika la DWWT kwa kuwahudumia wananchi kwa kutoa elimu ya kujikinga na maambikizi ya virusi vya UKIMWI ambapo maambukizi hayo yanazidi kupungua.
Naye Zawadi Jeremia ambaye ni mhudumu ngazi ya jamii ameshukuru kwa elimu waliyopatiwa na wataendelea kutoa elimu hiyo kwa wananchi wengine ili waweze kuchukua tahadhari ya kujinga na maambukiza ya virusi ya UKIMWI.
Buchosa District Council
Anuani: 44 Buchosa - SENGEREMA
Simu: 0759941297
Simu ya kiganjani: 0765029662
Barua pepe: ded@buchosadc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Hamlashauri ya Wilaya ya Buchosa. Haki zote zimehifadhiwa