Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Buchosa awataka watumishi wa Halmashauri kushirikiana na kupendana katika kufanya kazi ili kuleta ufanisi katika utendaji kazi Wilayani Buchosa Mkoani Mwanza.
Wito huo umetolewa leo na Mkurugenzi wa Halmashauri Wilaya ya Buchosa Bw.Benson Mihayo wakati akiongea na Watumishi wa Halmashauri makao makuu katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ambapo amewataka kufanya kazi kwa kushirikiana kwa pamoja ili kuleta ufanisi katika utendaji kazi.
Aidha Bw. Mihayo ameeleza na amefafanua kwamba Watumishi wanatakiwa kufuata sharia kanuni na taratibu za kazi pindi wanapotimiza majukumu yao ya kazi na kuahidi kushughulikia changamoto na kero za watumishi pindi zinapojitokeza.
Sambamba na hayo Mkurugenzi Mtendaji Bw.Mihayo amesisitiza na kuwashauri watumishi kuachana na tabia ya majungu na kusemana na badala yake wajishughulishe na fursa mbalimbali ambazo zinapatikana katika Hamasahuri hiyo ili kujikwamua kiuchumi.
Kwa upande wake Afisa Utumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Buchosha Bw.Ritte Adolph amewakumbusha watumishi kuzingatia sharia kanuni taratibu za kazi na kuwa na nidhamu ya kazi pindi wanapotimiza majukumu yao ya kazi ikiwa ni pamoja na kuwahi kazini na kutoka kazini muda uliopangwa.
Vilevile Bw.Adolph ametoa rai kwa watumishi wote Halmashauri ya Buchosa kuendelea kujifunza kwa bidii mfumo wa PEPMIS ambapo zoezi la kuingiza malengo katika mfumo bado linaendelea na kuwataka kutekeleza zoezi hilo likamilike kwa wakati.
Afisa Utumishi Mkuu wa Halmashauri ya Wilaya ya Buchosa Bw.Ritte Adolph (aliyesimama) akitoa maelekezo kwa Watumishi wakati wa kikao leo mapema katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ambapo aliwataka Watumishi kuzingatia nidhamu ya kazi pindi wanapo timiza majumu yao ya kila siku.
Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Buchosa wakifuatilia kwa makini katika kikao kilichofanyika leo mapema katika ukumbi wa Halmashauri ambapo wametoa kero na changamoto zao kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmasahuri ya Wilaya ya Buchosa.
Buchosa District Council
Anuani: 44 Buchosa - SENGEREMA
Simu: 0759941297
Simu ya kiganjani: 0765029662
Barua pepe: ded@buchosadc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Hamlashauri ya Wilaya ya Buchosa. Haki zote zimehifadhiwa