Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Buchosa afanya kikao na watumishi wa Halmashauri makao makuu na kuahidi kutatua changamoto zinazowakabili.
Mkurugenzi wa Halmashauri Wilaya ya Buchosa Bw.Benson Mihayo amefanya kikao leo tarehe 17,Disemba,2024, na Watumishi wa Makao makuu ikiwa ni utaratibu wake wa kawaida aliojiwekea wa kuongea na watumishi kila robo ya mwaka ambapo amesikiliza kero na changamoto mbalimbali zinazowakabili watumishi ikiwa ni pamoja na uhaba wa vitendea kazi,vyombo vya usafiri na madeni ya watumishi.
Bw. Mihayo ameeleza na kufafanua kwamba atahakikisha kila mtumishi anapata stahiki zake za msingi ikiwa pamoja na kulipa fedha za madeni ya uhamisho,likizo na safari kulingana na Bajeti ya Halmashauri itakavyokuwa inaimarika.
Aidha Mkurugenzi Mtendaji amesema atatua changamoto ya usafiri ikiwa ni pamoja na kutengeneza gari moja bovu na kununua pikipiki kadhaa ili kurahisha changamoto iliyokwepo ya baadhi ya watumishi kukosa usafiri wa kwenda kukagua miradi mbalimbali ya Maendeleo.
Hata hivyo,amewataka watumishi kuendelea kufaya kazi kwa juhudi na kwenye mfumo wa PEPMIS ili kuendana na kasi iliyopo na kila mtu atimize majukumu kwa nafasi yake.
Kwa upande wao watumishi wamefurahishwa na kitendo cha Mkurugenzi Mtendaji cha kuwa na utaratibu wa kuongea na watumishi na kusiliza changamoto zao.
Buchosa District Council
Anuani: 44 Buchosa - SENGEREMA
Simu: 0759941297
Simu ya kiganjani: 0765029662
Barua pepe: ded@buchosadc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Hamlashauri ya Wilaya ya Buchosa. Haki zote zimehifadhiwa