Mkuu wa Wilaya ya Sengerema awataka Watendaji wa Kata kusimamia kikamilifu zoezi la utoaji chakula katika Kata zao ili kuboresha Lishe na kupunguza udumavu kwa Watoto na kujenga taifa lenye afya njema katika Halmashauri ya Buchosa.
Mkuu wa Wilaya ya Sengerema Mhe Senyi Ngaga amewataka Maafisa na watendaji wa Kata kusimamia na kuhakikisha Watoto wa shule za Sekondari na Msingi wanapata chakula kwa asilimia 100 katika Halmashauri ya Buchosa.
Wito huo umetolewa leo tarehe 05, Novemba,2024 wakati wa akifungua kikao cha Tathmini ya utekelezaji wa mktaba wa shughuli za lishe katika Halmashauri ya Buchosa kwa kipindi cha Julai hadi Septemba 2024 ili kuongeza ufaulu,mahudhurio ya wanafunzi shuleni kwani lishe bora ina mchango mkubwa katika kufanikisha hayo.
Aidha Bi.Ngaga amepongeza na kutoa zawadi ya motisha kwa Kata tano (5) ambazo zimefanya vizuri katika uhamasishaji wa utoaji chakula shuleni ambapo Kata ya Nyakasungwa imeongoza kwa asilimia 100.94,Kata ya Kazunzu asilimia 100,Kata ya Kalebezo asilimia 100,Kata ya Maisome asilimia 76 na Kata ya Kasisa asilimia 67.84.
Watendaji wa Kata wakisikiliza na kupokea maelekezo katika kikao cha Tathmini ya utekelezaji wa Mkataba wa Lishe kipindi cha Julai hadi Septemba 2024 ambacho kimefanyika leo tarehe 5,Novemba,2024 katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri.
Buchosa District Council
Anuani: 44 Buchosa - SENGEREMA
Simu: 0759941297
Simu ya kiganjani: 0765029662
Barua pepe: ded@buchosadc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Hamlashauri ya Wilaya ya Buchosa. Haki zote zimehifadhiwa