Mkuu wa Wilaya ya Sengerema ameongoza Kikao cha Kamati ya Ushauri ya Wilaya (DCC) na kuwata viongozi na Watendaji kuwajibika katika kufanya kazi ili kuleta matokeo Chanya katika Halmashauri ya Buchosa.
Mkuu wa Wilaya ya Sengerema Mhe.Senyi Ngaga leo tarehe 17, Disemba,2024 ameongoza kikao cha Kamati ya Ushauri ya Wilaya katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Buchosa ambapo amewataka Watendaji na Viongozi mbalimbali kusimamia na kutekeleza majukumu kwa nafasi zao ili kuleta ufanisi na maendeleo katika Halmashauri ya Buchosa.
Mhe.Ngaga amesisitiza na kuwataka Viongozi na Wataalamu kufanya maandalizi yakinifu ya kuwapokea wanafunzi Januari,2025 wa darasa la Awali,la kwanza na wanafunzi wa kidato cha kwanza pindi watakaporipoti katika shule za Msingi na Sekondari.
Aidha amewakumbusha wazazi na walezi kutekeleza majukumu yao ya kuwahudumia watoto na kufanya maandilizi ya mahitaji ya msingi kwa wanafunzi kwa ajili ya kujiandaa na masomo pindi shule zitakapofunguliwa mwakani.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Hamashauri Mhe.Idama Kibanzi amewataka Viongozi na Wataalam kwa upande wa Sekta ya Elimu kusimamia kikamilifu sekta hiyo ili kuleta ufanisi na matokeo chanya.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Buchosa Bw.Peter Mihayo amesema kwamba atayafanyia kazi yote ya msingi kwa maendeleo ya Halmashauri ya Wilaya Buchosa.
Kikao hicho kimejadili taarifa za Maendeleo ya Halmashauri katika Sekta mbalimbali ikiwemo Maji,Umeme,Barabara zimejadiliwa,Sambamba na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali wa maendeleo wakiwemo Viongozi wa Siasa,Viongozi wa Dini na Viongozi wa Taasisi za Serikali.
Buchosa District Council
Anuani: 44 Buchosa - SENGEREMA
Simu: 0759941297
Simu ya kiganjani: 0765029662
Barua pepe: ded@buchosadc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Hamlashauri ya Wilaya ya Buchosa. Haki zote zimehifadhiwa