Mkuu wa Wilaya ya Sengerema ameongooza ziara ya kutembelea na kukagua miradi ya Maendeleo ambayo inapitiwa na mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2024 kwa ajili kufuatilia mafanikio na changamoto zilizopo ili kuhakikisha Mbio za Mwenge unapokelewa vizuri katika Halmashauri ya Buchosa.
Mkuu wa Wilaya ya Sengerema Mhe.Senyi Ngaga akiambatana na Kamati ya Ulinzi na Usalama kutoka Wilaya ya Sengerema amesema miradi yote inayopitiwa na Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2024 katika maeneo yote, Wataalamu na Watendaji wahakikishe mapungufu yote ya miradi inayojengwa yafanyiwe kazi na kuzingatia ubora na viwango na kuendana na thamani halisi ya fedha zilizotumika na wahusike wote wawajibike kikamilifu katika jukumu hilo la kitaifa.
Kwa upande wake Mratibu Msaidizi wa sherehe za mbio za Mwenge wa Uhuru katika Halmashauri ya Wilaya ya Buchosa Bw.Emmanuel Mtambulo kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri Bw.Benson Mihayo amewasilisha taarifa ya hali utekelezaji wa Miradi mbalimbali itakayotembelewa ambayo ni pamoja na miradi ya Sekta ya Elimu ikiwemo miundombinu ya vyumba vya madarasa,Sekta ya Afya,Sekta ya Maji,na Utunzaji wa Mazingira ambapo miradi hiyo kuwekewa jiwe la msingi,kukaguliwa pamoja kuzinduliwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Buchosa.
Aidha mbio za mwenge wa Uhuru kwa mwaka 2024 zinatarajiwa kukimbizwa katika Halmashauri 8 za Mkoa wa Mwanza kuanzia tarehe 6 Oktaba hadi tarehe 13, na sherehe za kuhitimisha Mbio hizo Kitaifa zitafanyika tarehe 14 Oktoba mwaka 2024 Jijini Mwanza,ambapo mbio za Mwenge zinakimbizwa kwa kaulimbiu ya Uhifadhi wa Mazingira na Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, ”Tunza mazingira na Shiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa ujenzi wa Taifa endelevu”.
Buchosa District Council
Anuani: 44 Buchosa - SENGEREMA
Simu: 0759941297
Simu ya kiganjani: 0765029662
Barua pepe: ded@buchosadc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Hamlashauri ya Wilaya ya Buchosa. Haki zote zimehifadhiwa