Mkuu wa Wilaya ya Sengerema Mhe. Senyi Ngaga awataka Watumishi kujenga mahusiano mazuri kazini ili kuleta ufanisi katika utendaji kazi katika Halmashauri ya Buchosa Mkoani Mwanza.
Mhe.Senyi Ngaga amebainisha hayo mapema leo tarehe 03, Aprili,2025 wakati akiongea na watumishi wa makao makuu katika Ukumbi wa mikutano ambapo amesisitiza mahusiano mazuri,ushirikiano na kupendana pindi wanapotimiza majukumu yao ya kazi.
Mhe. Ngaga amesema kwamba watumishi wanao wajibu wa kufanya kazi kwa bidii ili kuleta matokeo chanya katika taasisi za Serikali sambamba kupata stahiki zao za msingi ikiwa pamoja na kulipwa madeni ya uhamisho,likizo na ugonjwa pindi wanapokuwa kazini.
Aidha Bi.Nganga ametoa maelekezo kwa viongozi wakuu wa Idara na Vitengo kuendelea kufanya maandalizi ya ugeni wa Waziri Mkuu ambaye anatarajiwa kufanya ziara katika Halmashauri ya Buchosa hivi karibuni.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Buchosa Bw.Benson Peter Mihayo amewaomba watumishi kuendelea kufanya kazi kwa weledi na kujituma ,Serikali itaendelea kulipa stahiki mbalimbali za watumishi katika Halmashauri ya Wilaya ya Buchosa.
Buchosa District Council
Anuani: 44 Buchosa - SENGEREMA
Simu: 0759941297
Simu ya kiganjani: 0765029662
Barua pepe: ded@buchosadc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Hamlashauri ya Wilaya ya Buchosa. Haki zote zimehifadhiwa