Wagombea watatu kutoka vyama vya CHAUMMA, ADC na ACT Wazalendo wamejitokeza leo Jumatatu kuchukua fomu za uteuzi wa kugombea ubunge katika jimbo la Buchosa.
Wagombea hao Faustine Precide Ruhabuza (ACT Wazalendo), Esther Mussa Fulano (CHAUMMA) na Komanya Julius Athanas (ADC), wamekabidhiwa fomu hizo na Msimamizi wa Uchaguzi jimbo la Buchosa, Bw.Deogratius Lihengelimo.
Aidha makabidhiano hayo yamefanyika katika leo tarehe 25 June 2025 katika Ofisi ya Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Buchosa iliyopo Ofisi za Halmashauri ya Wilaya ya Buchosa.
Mgombea kupitia Chama cha ACT Wazalendo Bw.Faustine Ruhabuza (mkono wa kulia) akikabidhiwa fomu za uteuzi leo mapema katika Ofisi za Msimamizi wa Uchaguzi jimbo la Buchosa.
Mgombea kupitia Chama cha ADC Bw.Komanya Julius (Mkono wa kulia) akikabidhiwa fomu za uteuzi leo mapema katika Ofisi za Msimamizi wa Uchaguzi jimbo la Buchosa na Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Buchosa Bw.Deogratius Lihengelimo.
Mgombea kupitia Chama cha CHAUMMA Bi.Esther Fulano akijaza fomu za uteuzi leo mapema katika Ofisi za Msimamizi wa Uchaguzi jimbo la Buchosa.
Buchosa District Council
Anuani: 44 Buchosa - SENGEREMA
Simu: 0759941297
Simu ya kiganjani: 0765029662
Barua pepe: ded@buchosadc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Hamlashauri ya Wilaya ya Buchosa. Haki zote zimehifadhiwa