Disemba 9, kila Mwaka Tanzania Bara husherehekea Siku ya Uhuru wa Tanganyika uliopatikana Disemba 9, 1961 kutoka kwa Uingereza.
Halmashauri ya Wilaya ya Buchosa leo tarehe 9 Disemba,2024 imeadhimisha siku ya Uhuru wa Tanzania Bara katika Kata ya Nyakaliro kwa kufanya usafi wa mazingira na kupanda miti ambapo takribani miche 520 imepandwa katika Shule ya msingi Lumeya iliyopo Kata ya Nyakaliro.
Akiongea katika maadhimisho hayo Katibu Tawala wa Wilaya ya Sengerema Bw.Cuthbert Midala ambaye alimwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Sengerema amesema kuwa maadhimisho hayo yamejikita zaidi katika kufanya shughuli za kijamii kama kupanda miti na kufanya usafi wa mazingira ambapo kwa Wilaya ya Sengerema imefanya usafi katika hospitali ya Wilaya ya Sengerema na kwenye vituo vya na kupanda miti,kwaHalmashauri ya Buchosa imefanya usafi wa mazingira katika hospitali ya Wilaya Isaka iliyopo Kata ya Nyehunge pamoja na upandaji miti.
Aidha Bw.Midala ametoa wito kwa wananchi kuendelea kutunza mazingira kwa kufanya usafi wa mazingira pamoja na kupanda miti na kuilinda ili ilete manufaa kwa wananchi na vizazi vijavyo.
Kwa upande Mhifadhi Mkuu wa TFS Sengerema Bw.Steven Odongo Oyugi ameeleza na kufafanua kwamba wao kama TFS wanatoa elimu kwa wananchi namna nzuri ya kupanda na kuitunza miti na kutunza mazingira kwa ujumla wake pamoja na kugawa miche mbalimbali, ambapo ametoa wito kwa wananchi Kwenda kuchukua miche kwa ajili kupanda kwa manufaa ya wananchi kwa kujipatia kipato.
Vilevile Diwani wa Kata ya Nyakaliro Mhe.Paulo Kabugwe ametoa shukrani za pekee kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano Mhe.Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuleta fedha kwa ajili ya kutekeleza miradi ya maendeleo katika Halmashauri ya Buchosa na Kata ya Nyakaliro.
Naye mkazi wa Kijiji cha Lumeya Bw.Edward Mazengo ameomba uongozi wa TFS kuendelea kutoa elimu kwa wananchi juu umuhimu wa kutunza mazingira hasa upandaji wa miti ili kunusuru majangwa ambayo yanaendelea kutokea katika maeneo yanayowazunguka.
Katika maadhimisho hayo wananchi wamejitokeza kwa wingi katika kuadhimisha miaka 63 ya Uhuru Tanzania Bara ambapo kauli mbiu inasema “Uongozi Madhubuti na Ushirikishwaji wa Wananchi ni Msingi wa Maendeleo yetu”.
Buchosa District Council
Anuani: 44 Buchosa - SENGEREMA
Simu: 0759941297
Simu ya kiganjani: 0765029662
Barua pepe: ded@buchosadc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Hamlashauri ya Wilaya ya Buchosa. Haki zote zimehifadhiwa