Baraza la Wafanyakazi la Halmashauri ya Wilaya ya Buchosa lajadili na kupitisha mapendekezo ya Bajeti ya Mapato na Matumizi ya shilingi Bilioni 42.4 kwa mwaka wa fedha 2025/2026 Wilayani Buchosa Mkoani Mwanza.
Kikao maalum cha Baraza la Wafanyakazi kwa ajili kutoa mapendekezo ya bajeti katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ambapo Mwenyekiti wa kikao hicho ambaye pia ni Afisa Utumishi wa Halmashauri ya Buchosa Bw. Adolf Ritte ameeleza kwamba ni halali kwa kila mfanyakazi kutimiza wajibu wake na kusisitiza ushirikiano ili kuhakikisha wanafikia adhima na malengo yaliyowekwa na kuwaomba Watumishi waendelee kutekeleza majukumu kwa kuzingatia Bajeti iliyopitishwa.
Bw. Adolph amefafanua na kueleza kuwa kikao hicho ni maalum kwa ajili ya kupitia,kujadili na kufanya tathmini ya utendaji kazi ambapo kila mfanyakazi ana haki katika utekelezaji wa majukumu na stahiki anapowajibika kutimiza malengo yaliyopangwa kwa mwaka wa fedha 2025/2026.
Awali akiwasilisha rasimu ya Bajeti ya mwaka 2025/2026 Afisa Mipango wa Halmashauri Bw.Deogratius Ihengelimo kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Buchosa amefafanua kwamba katika rasimu hiyo ya Bajeti kiasi cha shilingi 4,311,199,797.00/= ni fedha zitokanazo na vyanzo vya Mapato ya ndani ya Halmashauri ,kiasi cha shilingi. Bilioni 25,538,180,000/= ni fedha ya mishahara ya Watumishi, na kiasi cha shilingi Bilioni 2,107,638,000/= ikiwa ni ruzuku ya uendeshaji (OC) na kiasi cha shilingi Bilioni 10,458,340,000/= ni kwa ajili ya kutekeleza Miradi ya Maendeleo na fedha zote ni kutoka Serikali kuu.
Aidha Bw.Ihengelimo ameeleza kuwa pamoja na kuwepo kwa rasimu ya bajeti hiyo ofisi ya Mipango na Uratibu imeahidi kutekeleza na kufanyia kazi mapendekezo na maadhimio ya kikao hicho ikiwa ni pamoja na kuendeleza ushirikiano ili kuhakikisha kuwa na maendeleo chanya katika jamii ndani ya Halmashauri ya Buchosa.
Hata hivyo kupitia kikao hicho cha Baraza la Wafanyakazi, wajumbe walipata wasaa wa kupitia na kujadili pamoja na kutoa maoni yao juu ya Bajeti hiyo na kupongeza namna ulivyoandaliwa kitaalamu.
Buchosa District Council
Anuani: 44 Buchosa - SENGEREMA
Simu: 0759941297
Simu ya kiganjani: 0765029662
Barua pepe: ded@buchosadc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Hamlashauri ya Wilaya ya Buchosa. Haki zote zimehifadhiwa