Bazara za Madiwani la ridhishwa na kupongeza taarifa za hesabu za mwisho kwa mwaka wa fedha ulioishia Juni 30, 2024 katika Halmashauri ya Wilaya ya Buchosa.
Pongezi hizo zimetolewa leo 28,Agosti,2024 ambapo Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Buchosa na diwani wa Kata ya Nyazenda Mhe.Idama Kibanzi ameeleza na kufafanua kwamba Baraza la Madiwani katika kikao chake cha kujadili taarifa za hesabu za mwisho kwa mwaka wa fedha ulioishia Juni 30, 2024 limeridhika na taarifa hiyo ambayo imeeleza kila kitu kwa undani na kwa ufasaha kwa kuzingatia viwango vya kimataifa vya uandaji wa hesabu za Sekta za Umma.
“Kwa mwaka huu naona hesabu zetu ziko salama,nawashukuru Madiwani,Mkurugenzi Mtendaji na menenjimenti kwa namna ya pekee unavyoonesha ushirikiano kwa waheshimiwa Madiwani”.Ameongeza Mwenyekiti wa Halmashauri ya Buchosa Mhe.Kibanzi.
Aidha Bw.Kibanzi amesema kwamba taarifa za hesabu kwa mwaka wa fedha 2023/2024 zimejumuisha mapato,matumizi,mali za kudumu,madeni,mali zilizo salia stoo na salio la fedha kwenye akaunti za Halmashauri,shule,Zahati,Vituo vya Afya,Kata na Vijiji.
Katika Hatua nyingine Baraza la Madiwani kwa ujumla wake limeridhia na kumpongeza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Buchosa Bw.Benson Mihayo kwa namna anavyosimamia na kushirikiana na Madiwani pamoja na namna taarifa ilivyoandaliwa kitaalamu kwa kuzingatia vigezo vya Kimataifa na kujumuisha vitu vya msingi ikiwa pamoja na madeni ya watumishi na wazabuni wanaoidai katika Halmashauri ya Wilaya ya Buchosa.
Kwa upande wake Kaimu Mkuu mweka Hazina CPA Justice N.Shemakange amesema uandaji wa hesabu za kuishia 30/06/2024 umezingatia viwango vya kimataifa vya uandaji wa hesabu za Sekta Umma,sheria za fedha ,sharia za manunuzi ya umma ya mwaka 2011 na kanuni zake za 2013 na 2016 na sheria ya Serikali za mitaa ya mwaka 1982 kama ilivyorekebishwa mwaka 2000.
Hata hivyo,Bw.Shemakange ametoa shukrani za pekee kwa menejimenti ya Halmashauri ya Wilaya ya Buchosa na Kitengo cha fedha kwa ushirikiano wa dhati walioonesha kwa kipindi cha maandalizi ya hesabu hizo zilizoishia Juni,30,2024.
Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Buchosa leo limejadili na kuridhwisha na taarifa ya hesabu za mwisho kwa mwaka wa fedha ulioishia Juni 30,2024 katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri.
Kaimu Mkuu mweka Hazina wa Halmashauri ya Wilaya ya Buchosa CPA Justice N.Shemakange akiwasilisha taarifa za hesabu za mwisho wa mwaka ambapo amesema uandaji wa hesabu za kuishia 30/06/2024 umezingatia viwango vya kimataifa.
Buchosa District Council
Anuani: 44 Buchosa - SENGEREMA
Simu: 0759941297
Simu ya kiganjani: 0765029662
Barua pepe: ded@buchosadc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Hamlashauri ya Wilaya ya Buchosa. Haki zote zimehifadhiwa