Wananchi wa Kijiji cha Bilulumo Kata ya Kafunzo Halimashauri ya Buchosa Wilayani Sengerema Mkoani Mwanza wameitikia agizo la Rais wa Jahuri ya Muungano wa Tanzania kwa kukamilisha zoezi la upatikanaji wa madawati katika shule yao.
Kauli hiyo imetolewa na Diwani wa Kata ya Kafunzo Dotto Bulunda alipokuwa akizungumuza wa waandishi wa habari walipotaka kujua katika Kata yake amejipangaje kumaliza tatizo la madawati katika shule za msingi na Sekondari zilizopo katika kata yake.
Alisema kuwa Kata ya Kafunzo inaundwa na Vijiji Vitatu ambavyo ni Bilulumo, Luhorongoma na Kafunzo ambapo Kata hiyo ina shule tatu za msingi na Sekondari moja na hadi sasa hadi sasa Shule ya Msingi ambayo imekamilisha madawati ni moja shule ya msingi Bilulumo ambayo wananchi wake wamejitoa kwa moyo na kukamilisha swala hilo.
Bulunda alisema jitihada za kuhamasisha wananchi na wao wakaitiki kwa kujitoa ndiyo imesabisha jamii kuona umuhimu na kumalisha swala hilo ambapo hadi sasa mahitaji ya shule hiyo upande wa madawati ili kuwa ni madwati miatatu na kumi[310] hadi sasa wamevuka lengo na kiufikisha madawati miatatu ishirini na tano[325] na wamekuwa na ziada.
‘’ Ninatumia furusa hii kuwaomba wananchi wa vijiji vya Kafunzo na Luhorongoma wajitoe kwa moyo nao wakamilishe swala hilo katika muda uliopangwa litakuwa jambo jema na lenye tija kwa jamii nzima hivyo kila mmoja wajibike kwa nafasi yake na kutimiza kile walichokubaliana ili kumaliza tatizo la madawati katika shule zetu , katika shule ya Sekondari hatuna upungufu wowote , Alisema Bulunda.
Mwenyekiti wa Kijiji cha Bilulumo Kambona Bulela alisema siri ya mafaniko ya kufanikisha zoezi hilo ni kuwekana wazi katika vikao vya kijiji na kukubaliana ambapo walitumia miti shule kuengeneza madwati themanini na wananchi walichangia madawati themanini na tatu na kumaliza upungufu huo.
Mwalimu wa Shule ya Msingi Bilulumo Said Malekela alisema kuwa mahusiano mazuri ya walimu na wananchi pamoja na uhamasishaji wa Diwani wa Kata hiyo katika swala la maendeleo ndiyo imekuwa chachu ya kufanikisha zoezi hilo na kukamilisha swala la upatikanaji wa madawati katika shule hiyo ambapo shule hiyo ina jumla ya wanafunzi mia tisa thelathini na mbili kuanzia darasa la awali hadi darasa la saba hakuna mwanafunzi ambaye anakaa chini kwa kuwa shule hiyo ilikuwa na uhitaji wa madawati 310 na yamekamilika yote na inaziada ya dawati 25.
Buchosa District Council
Anuani: 44 Buchosa - SENGEREMA
Simu: 0759941297
Simu ya kiganjani: 0765029662
Barua pepe: ded@buchosadc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Hamlashauri ya Wilaya ya Buchosa. Haki zote zimehifadhiwa