Harakati za kupambana juu ya upatikanaji wa chakula shuleni kupitia hamasa mbalimbali ili watoto waweze kupata mlo kamili pamoja na kusoma katika mazingira mazuri katika Halmashauri ya Buchosa.
Mkuu wa Wilaya ya Sengerema Mhe.Senyi Ngaga leo tarehe 17,Septemba,2025 akizungumza na Watendaji wa wa Kata katika kikao cha Tathmini ya utekelezaji wa mkataba wa Lishe ambacho kimefanyika katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri amepongeza juhudi za kuhakikisha hali ya upatikanaji wa chakula shuleni ambapo imeongezeka ukulinganisha na hapo awali kwa kutumia mbinu mbalimbali.
Aidha Bi.Ngaga amesisitiza na kuwaataka watendaji wa Kata zote za Halmashauri kufanya jitihada za kuongeza hali ya upatikanaji wa Lishe mashuleni kwa kuwahamasisha wazazi ili kupunguza changamoto za Lishe katika Halmashauri ya Buchosa.
Aidha lengo la kikao hicho ilikuwa ni kupima hatua zilizofikiwa katika uboreshaji wa hali ya upatikanaji wa Lishe shuleni ambapo kwa Halmashauri ya Buchosa ina wastani wa asilimia 98.51 ambayo ni rangi ya kijani inayoonesha uhai au maendeleo mazuri ya utoaji wa huduma ya chakula.
Hata hivyo Kata tano zilizofanya vizuri katika kuhamasisha utoaji wa huduma ya chakula shuleni zimepokea fedha taslimu ikiwa lengo ni kutoa motisha kwa watendaji wa Kata hizo ambazo ni Kata ya Nyakasungwa,Nyazenda,Luharanyonga,Bulyaheke na Nyakaliro.
Buchosa District Council
Anuani: 44 Buchosa - SENGEREMA
Simu: 0759941297
Simu ya kiganjani: 0765029662
Barua pepe: ded@buchosadc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Hamlashauri ya Wilaya ya Buchosa. Haki zote zimehifadhiwa