Wananchi wa Visiwa vya Kome na Maisome na kunufaika na huduma usafiri wa haraka ili kunusuru Vifo vya Mama na mtoto katika Halmashauri ya Wilaya ya Buchosa mkoani Mwanza.
Kupitia Baraza la Madiwani ambalo limejadili taarifa za Kata kwa robo ya kwanza kipindi cha Julai hadi Septemba 2024/2025 limefanyika leo tarehe 07, Novemba ,2024 ambapo baraza la Madiwani limewasilisha taarifa za Maendeleo za Kata sambamba na changamoto zilizojitokeza katika kata zao.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Buchosa Mhe. Idama Kibanzi ameeleza na kufafanua katika mkutano wa baraza la Madiwani kwamba kuna umuhimu wa kutazama upya huduma ya usafiri wa haraka katika Visiwa vya Kome na Maisome ili kupata vivuko vipya ambavyo vitasaidia na kurahisiha huduma ya usafiri kwa wagonjwa hasa wamama wajawazito na kuwaondelea usumbufu wa kuvuka maji pindi wanapoenda sehemu nyingine kupata huduma ya afya.
Aidha Mhe.Idama amewataka Watendaji wa Taasisi za umma kuhakikisha wanasimamia na kutekeleza kikamilifu Miradi yote kama ilivyopangwa ili wananchi waweze kunufaika na matunda ya miradi hiyo ambayo Serikali inatoa fedha nyingi kwa ajili ya kutekeza miradi hiyo.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Buchosa Bw.Benson Peter Mihayo amesema kuwa Halmashauri imepeleka maombi kwa ajili kupata ambulace mbili ambapo moja itatumika katika kisiwa cha Kome na nyingine itatumika katika kisiwa cha Maisome na tayari mchakato huo upo katika hatua nzuri.
Hata hivyo Waheshimiwa Madiwani wa Halmashauri ya Buchosa wameishukuru na kuipongeza Serikali ya awamu ya sita kwa kutoa fedha nyingi kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya Maendeleo katika kata zao ikiwemo miradi ya Sekta ya afya,Maji,Elimu na Miundombinu ya Barabara.
Mkutano huo wa Baraza la Madiwani umehudhuriwa na Viongozi wa Serikali Pamoja na Viongozi wa Chama cha Mapinduzi ,Waatalamu kutoka katika Idara na Vitengo Pamoja na wadau mbalimbali katika Halmasahuri ya Buchosa.
Waheshimiwa Madiwani wa Halmashauri ya Buchosa wakipitia na kujadili hoja mbalimbali leo tarehe 07,Novemba,2024 katika Mkutano wa Baraza la Madiwani katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri.
Wakuu wa Idara na Vitengo wakifuatilia kwa makini hoja mbalimbali na taarifa katika kikao cha Baraza la Madiwani ambacho kimefanyika leo mapema katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri.
Buchosa District Council
Anuani: 44 Buchosa - SENGEREMA
Simu: 0759941297
Simu ya kiganjani: 0765029662
Barua pepe: ded@buchosadc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Hamlashauri ya Wilaya ya Buchosa. Haki zote zimehifadhiwa