Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu amezindua chumba cha kuhifadhia majokofu yanayotumia nishati ya jua (umeme wa jua) kwenye Zahanati ya Nyakasungwa Halmashauri ya Wilaya ya Buchosa.
Halmashauri ya Buchosa imepata majokofu 17 kutoka Wizara ya Afya mwezi Oktoba 2019 kwa awamu ya kwanza na tayari yamesambazwa na kufungwa kwenye vituo vya kutolea huduma za afya.
Majokofu hayo yatasaidia kuimarisha mnyororo baridi na kuongeza ubora wa utunzaji wa chanjo katika vituo vya kutolea huduma za afya ambapo itapelekea watoto kupata chanjo zenye ubora kama ilivyokusudiwa
Hali ya chanjo kwa Halmashauri hiyo kwa mwaka huu ni asilimia 94 kutoka asilimia 79 mwaka jana na katika kampeni ya kitaifa ya chanjo ya Surua na Rubella mwezi Oktoba mwaka huu imefanikiwa kwa asilimia 106.
Pia waziri amatembelea kituo cha Afya Kome ambapo alipata wasaa wa kukagua chumba cha kutolea huduma za Upasuaji.
Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia wazee na watoto Ummy Mwalimu akiangalia maandalizi ya huduma za upasuaji kituo cha Afya Kome halmashauri ya Buchosa.
Buchosa District Council
Anuani: 44 Buchosa - SENGEREMA
Simu: 0759941297
Simu ya kiganjani: 0765029662
Barua pepe: ded@buchosadc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Hamlashauri ya Wilaya ya Buchosa. Haki zote zimehifadhiwa