Kitengo cha Makaguzi wa ndani kinasimamiwa na Erick Lubeya
MAJUKUMU YA KITENGO CHA UKAGUZI
Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani kina jukumu la kutoa angalizo na ushauri kwa taasisi kuhusiana na jinsi taasisi inavyotekeleza majukumu yake ya msingi. Huduma za ushauri ambazo Kitengo huzitoa ni zile zenye lengo la kuongeza ufanisi wa Taasisi.
Kwa upande wa Halmashauri za Serikali za Mitaa, wakaguzi wa ndani wanatoa maangalizo na ushauri wenye lengo la kuboresha huduma zitolewazo kwa wananchi. Ushauri na maangalizo haya yanapaswa kutolewa kwa uhuru na yanalenga kuiwezesha Halmashauri kufikia malengo ambayo imejiwekea. Majukumu ya Wakaguzi wa ndani yanapaswa kutekelezwa kwa utaratibu uliopangwa vizuri na wenye kuzingatia miiko ya taaluma na kwa kuzingatia misingi ya utawala bora.
LENGO KUU
Lengo kuu la ukaguzi ni kuona kama mifumo mbalimbali ya udhibiti iliyowekwa inafanya kazi kama ilivyokusudiwa. Kitengo cha Ukaguzi wa ndani kinafanya kazi zake kwa kuchambua mifumo ya udhibiti na kufanya tathmini ya kiwango cha uzingatiwaji wa mifumo hiyo katika utekelezaji wa majukumu ya siku kwa siku na kisha kutoa ushauri na maangalizo.
Buchosa District Council
Anuani: 44 Buchosa - SENGEREMA
Simu: 0625826705
Simu ya kiganjani: 0765029662
Barua pepe: ded@buchosadc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Hamlashauri ya Wilaya ya Buchosa. Haki zote zimehifadhiwa